Jumla ya Watahiniwa 10,021 Manispaa ya Morogoro wanatarajia kufanya mitihani ya Taifa ya kidato cha nne itakayoanza Novemba 4 mwaka huu Nchini kote.
Kati ya watahiniwa hao, Wavulana ni 4479 na Wasichana ni 5542 na Manispaa ya Morogoro ina kituo teule kimoja kilichopo katika Ofisi ya Manispaa na itakuwa na jumla ya Vituo 75. Miongoni mwa vituo hivyo 23 ni vya Shule za Sekondari za Serikali, Vituo 27 ni vya Shule za Sekondari za Binafsi,vituo 25 ni vya kujitegemea
Akieleza kuhusu maandalizi ya mitihani hiyo Afisa Elimu Sekondari Dkt.Janet Barongo ameeleza kuwa maandalizi yako vizuri na usimamizi na uendeshaji wa mitihani utazingatia watahiniwa waliosajili kufanya mtihani kwa kutumia fomu za Individual Attendance List(ISAL)
Aidha alitoa wito kwa watahiniwa kuhakikisha wanafika katika vituo vya mitihani mapema na kufuata sheria na kanuni zote za mitihani ikiwemo kuvaa sare kamili za shule.
Mbali na hayo aliwaasa wazazi kuwatia moyo wanafunzi na kuhakikisha wanafunzi wanapata chakula katika kipindi chote cha mitihani na kutowasumbua wanafunzi katika kipindi chote cha mitihani.
Pia Dkt Barongo aliwasihi walimu kuwa pamoja na wanafunzi wao na kuwatia moyo ili wafanye mitihani katika hali ya utulivu.
Dkt Barongo aliwatakia heri wanafunzi wote wanaofanya mitihani ya kidato cha nne kwa mwaka huu.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa