Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro , Emmanuel Mkongo, alipotembelea Mabanda ya Taasisi za umma na binafsi zinazojihusisha na shughuli za Kilimo, Mifugo na uvuvi kwenye viwanja vya Nanenane Kambarage Nyerere Mkoani Morogoro.
"Tumieni siku hizi nane za maonesho haya kuja kuchukua teknolojia kwenye maonesho haya. Mtu akifika hapa ataondoka na kitu, hapa watakuja watu kutoka Mataifa mbali mbali hivyo sisi wenyeji tunapaswa kuwa mstari wa mbele" Amesema Mkongo.
Mkongo, amesema wakulima na wafugaji wakienda kufanyia kazi teknolojia hiyo hata kwa asilimia 40 tu, wataweza kubadilisha maisha yao pamoja na uchumi na kuifanya Tanzania kuwa Kapu la chakula la Afrika kama ilivyo dhamira ya Mhe. Rais.Dkt. Samia Suluhu Hassan.
"Kiukweli nawashauri wananchi wenzangu waje wajionee mambo mazuri yanayopatikana hapa 88 kwenye mabanda mbalimbali haswa wafugaji wenzangu njooni mjifunze namna ya kufuga kisasa yaani ufugaji wenye tija kwa sababu kuna wataalamu wabobezi wa masuala haya watakuelekeza namna bora ya kufuga kisasa na kunufaika na kuacha mazoea ya ufugaji holela usiokuwa na tija" Ameongeza Mkongo.
Kauli Mbiu ya mwaka 2024 ni : “Chagua Viongozi Bora wa Serikali za Mitaa kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi”
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa