Wananchi na wakazi wa manispaa ya Morogoro wameendelea kujifunza shughuri mbalimbali za kilimo,Uvuvi na Ufugaji bora katika banda la manispaa ya morogoro katika Viwanja vya Mwl.Julius Nyerere.
Hayo yamethibitishwa na wananchi waliofika katika eneo la vipando la Manispaa ya Morogoro na kuvutiwa na Elimu ya kilimo cha kisasa inayotolewa na wataalamu wa kilimo na ufugaji ikiwemo elimu juu ulimaji wa mbogamboga,kilimo cha maghorofani,ufugaji bora wa samaki na kuku.
Aidha wananchi wamepata fursa ya kujionea kaushio la mbogamboga ambalo linatumia mwanga wa jua
Akizungumza na kutoa elimu Bibi Mwakaaje Mrisho ambae ni Mwenyekiti wa kikundi cha Green Voice kinachotokea kata ya kauzeni amesema kaushio hilo ambalo linatumia mwanga wa jua kukaushia mbogamboga lina faida nyingi hasa kwa wakina mama.
Bi Mrisho ameeleza kuwa kuna kipindi mavuno ya mbogamboga hupatikana kwa wingi sana kiasi ambacho mkulima hawezi kuuza kwa wakati mmoja,hivyo kwa kutumia kaushio hilo mkulima huweza kuzihifadhi kwa ajili ya kuuza mboga hizo kwa badae.
Aidha Bi Mrisho ameongezea kwa kusema kuwa ukaushaji wa mboga ni mzuri sana kwa kuwa huweza kumsaidia mwanamke kupata mboga kwa wakati na pia kujiongezea kipato .
Pia ameeleza kuwa mboga zinazokaushwa kwa kutumia kaushio hilo ubaki na ubora wake kwa muda wa mwaka mzima na kuwaomba wananchi wazidi kumiminika kujifunza zaidi.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa