Vikundi 101 vikiwemo 70 vya wanawake na vingine vya vijana katika Manispaa ya Morogoro vimepatiwa mikopo ya jumla ya Sh milioni 204.5 kwenye utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha wa 2017/2018.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, John Mgalula alisema hayo wakati akielezea baadhi ya mafanikio yaliyotokana na utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha wa 2017/2018.
“ Tumetoa mikopo ya jumla ya Sh 204,500,000 kwa ajili ya wanawake na vijana ambapo jumla ya vikundi 70 vya wanawake na 31 vya vijana walipatiwa mikopo” alisema Mgalula.
Mbali na mikopo alitaja mafanikio mengine ni ujenzi na ukarabati wa mabanda 14 na vizimba katika soko la Mawenzi , uendelezaji wa vituo vya Afya katika kata za Mafiga, Sabasaba , Kingolwira na Mafisa , pia kituo cha afya sina, Kihonda na Lukobe.
Pia alitaja mafanikio hayo ni pamoja na kuwezesha kaya masikini 2,621 katika Kata 29 za Manispaa ya Morogoro na kununuliwa kwa mapipa ya taka na kusambazwa katika vituo vya kukusanyia taka kwenye kata 13 kati ya 29 za Manispaa.
Katika hatua nyingine, Mkuu wa wilaya ya Morogoro, Regina Chonjo amewataka wananchi wa Manispaa kulinda miundombinu ya barabara zilizojengwa kwa fedha za mikopo na kuwafichua wahujumu wa miundombinu hiyo ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria .
Mkuu huyo alitoa rai hiyo katika kikao hicho cha Kamati ya Ushauri ya wilaya baada ya watu wasiofahamika kung’oa taa saba za sola katika barabara ya kisasa iliyojengwa kwa kiwango cha lami nzito katika barabara ya Nane Nane .
“ Taa hizi za sola ni za kisasa na thamani ya taa moja ni Sh milioni nne na zaidi , watu wameziiba na kuisababishia hasara serikali na wananchi kwani hizo ni kodi za watanzania , lazima tuwafichue watu hawa waovu” alisema Chonjo.
Mkuu wa wilaya alisema , licha ya wizi wa taa hizo pia watu wasiofahamika wamevunja silingi bodi katika baadhi ya vyumba vya madarasa ya shule ya Sekondari Mgulasi na kuondoka nazo.
“ Naomba hapa kuna viongozi wa dini na wa vyama vya siasa , tuwe mabalozi wa kutoa elimu kwa wananchi kuwa miradi hii imejengwa kwa gharama kubwa na inatokana na fedha za kodi za watanzania , hatuna budi kuilinda na kuwafichua wahalifu hawa “ alisema Chonjo.
Naye mkazi wa Manispaa hiyo, Sakina Bakari licha ya kujitokeza kwa wizi wa taa za barabarabani aliiomba halmashauri kuangalia barabara zenye uhatarishi nyakati za usiku na kuziwekea taa
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa