Walengwa wa TASAF Manispaa ya Morogoro wametakiwa kujisajili katika mfumo wa mtandao ili kuweza kulipwa malipo yao.
Kauli hiyo imetolewa na Mratibu wa TASAF Manispaa ya Morogoro, Bi Feliciana Katemana wakati wakifanya malipo kwa wanufaika hao wa mfuko wa TASAF.
Akizungumza na Wanufaika hao, Katemana, amesema mfumo huo wa malipo kwa njia ya mtandao utarahisisha upatikanaji wa malipo kwa urahisi tofauti na kuwafuata walengwa mahali walipo kutokana na miundombinu.
Aidha, amewataka walengwa wote wa mfuko wa TASAF ambao bado hawajaingia katika mfumo wa usajili kwa njia ya mtandao wajisajili mapema ili wakati wa malipo waweze kupatiwa stahiki zao.
‘’ Tunashukuru kwa kuwepo kwa mfumo mpya wa malipo ya mtandao kwani mpango huu sisi ni mara ya kwanza kulipa kwa njia hii ni mzuri na salama kwa walengwa na wawezeshaji na kuna urahisi wa malipo tofauti na kuwafuata walengwa mahali walipo kutokana na miundombinu lakini kupitia mtandao tunaweza kufanya malipo kwa haraka zaidi niwaombe Wenyeviti wa Mitaa, Watendaji wa Mitaa, Kata kuwahamasisha walengwa wajisajili na mtandao kwa kutumia simu au benki wale amabao watakosekana katika uhakiki watakuwa wamejiondoa wenyewe katika mpango huu” Amesema Katemana.
Hata hivyo , Katemana ,amesema kuwa katika kipindi hiki wamepokea jumla ya shilingi 108,352,120 millioni kwa jili ya wanufaika wa TASAF na shilingi 60,846,120 millioni zimelipwa kwa njia ya mtandao na shilingi 47,506,000 zimelipwa kwa pesa taslimu kwa sababu kuna walengwa wamejisajili na mtandao lakini majina yao waliojisajili nayo kwenye mpango wa TASAF hayafanani na majina yaliyo kwenye kitamburisho cha Taifa au cha mpiga kura.
Aidha, amesema kuwa mpaka sasa jumla ya walengwa 6561 wameshatambuliwa kupitia ngazi ya mtaa na kuwasilisha idadi hiyo makao makuu na mwezi juni 2021 hivyo kinachofanyika sasa ni kufanya utambuzi yakinifu wa 30% na utambuzi huu utafanyika kwanjia ya mikutana hivyo walengwa wote wakati wa kitishwa mikutano wanatakiwa kujitokeza na kutambuliwa kwa kushirikiana na viongozi wa Mtaa, Kata na wananchi wenyewe kama ilivyo kuwa miaka mingine iliyopita.
Mbali na hayo Katemana amesema kutafanyika zoezi la utambuzi wa 30% wa kaya zilizo katika mpango wa TASAF kwani mpango wa awamu ya pili ulifika kwa asilimia 70% na mwezi juni utambuzi wa asilimia zilizobaki utafanyika huku wananchi wakitakiwa kutoa mchango wao wa kuwatambua wenzao kwani wao ndiyo wanawajuwa watu wao kupitia vigezo ambavyo vinatumika kuwatambua wanufaika hao.
Mpaka sasa jumla ya walengwa 2504 wameshalipwa malipo yao ambapo walengwa 1190 wamelipwa kwa fedha taslimu na walengwa 1314 wamelipwa kwa njia ya mtandao.
Mwisho,amewataka , wanufaika wote wa TASAF , kutumia fedha wanazo pata kwa manufaa ili waweze kujiwekeza zaidi kupitia fedha hizo na kuachana na mambo ya hanasa kwani fedha hizo ni kwaajili ya kujinasua na umaskini kwa kujishughulisha na shughuli mbalimbali za kiujasiliamal
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa