Msaada huo umekeabidhiwa Juni 30/2023 kwa Kaimu Mganga Mfawidhi huku Diwani wa Kata ya Mafiga Mhe. Thomas Butabile akiongoza Kikundi hicho pamoja na Viongozi wa Chama na Serikali.
Akizungumza wakati akikabidhi msaada, Mwenyekiti wa Kikundi hicho, Mwanahamisi Juma , amesema wanamshukuru Mwenyezi Mungu wameweza kuwa sehemu ya kupata wasaa wa kutoa msaada huo waliobarikiwa kutoa katika wodi ya Wazazi.
Awali akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo, Kaimu Mganga Mfawidhi wa kituo hicho , Neema Mkuya ambaye pia ni Nesi katika Wodi ya Wazazi, amekishukuru Kikundi hicho kwa kuona umuhimu wa kuwasaidia msaada huo ambao umefika wakati muafaka.
“Nashukuru kupokea neema ambazo mmezileta Wana tupendane,natoa shukrani zangu za dhati kwa ajili ya zawadi na wagonjwa wetu ambao wanajiandaa kupata watoto na wale ambao wameshapata watoto ”Amesema Semkuya.
Mmoja wa wazazi waliopokea msaada wa sabuni, amekishukuru Kikundi cha wakina mama hao na kuwaomba kuendeleza moyo wa kutoa kidogo wanachojaaliwa kusaidia wenye uhitaji.
Naye Diwani wa Kata ya Mafiga, Mhe. Thomas Butabile, amekipongeza Kikundi hicho cha wakina mama kwa masaada wao huku akiomba wadau wengine kujitokeza kutoa misaada kwani Serikali pekee haiwezi kukidhi huduma zote katika kuimarisha huduma ya afya.
Ili kuona Kikundi hicho kinapiga hatua, Mhe. Butabile, amehaidi kuwapa shilingi 200,000/= kwa ajili ya kuongeza mtaji wa Viti kwa kikundi hicho.
“Tunajua msaada huu ni mdogo sana ukilinganisha na mahitaji yaliyopo, lakini tunaamini itasaidia na tunawaomba wengine kujitolea kusaidia kila mmoja kwa uwezo wake, nimeona jitihada zenu na mimi ili kuwaunga mkono nitawapa laki 2 muendeleze mradi wenu wa Viti na katika shughuli zetu nimeagiza Uongozi wa Kata uje kukodi vitu hapa ili tuendelee kuwashika mkono ”Amesema Mhe. Butabile.
Naye Mtendaji wa Kata ya Mafiga, Amina Saidi, amewapongeza wakina Mama hao kwa uthubutu wa kuanzisha kikundi na kujiendesha wenyewe pasipo na mkopo kutoka Serikalini.
Afisa Maendeleo ya Jamii Kata ya Mafiga, Mwaru Kizega, amesema katika mikopo ijayo kikundi hicho kinastaili mkopo kwani wameonesha imani kubwa kwamba hata wakipewa mkopo wanauwezo wa kurudisha kwani wameanza miradi na fedha zao jambo ambalo linafaa kuigwa kwa vikundi vyengine.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Mafiga A, Ndg. Fadhili Dutilo, ameushukuru Uongozi wa Kata wakiongozwa na Diwani kwa kukubali kuhudhuria katika hafla ya Kikundi hicho huku akiahidi kuendelea kutoa ushirikiano na Vikundi ambavyo vitaanzishwa vyenye lengo la kujikomboa na kujkwamua kiuchumi.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa