Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Suleiman Jafo amekagua mradi wa barabara yenye urefu wa Km.4.6 iliyopo Manispaa ya Morogoro uliogharimu shilingi Bil. 12.6 ikiwa ni utekelezaji wa uboreshaji miji (ULGSP).
Akikagua Mradi huo Waziri Jaffo alisema kuwa lengo la kukagua mradi wa barabara ya Tubuyu,Nanenane na Maelewano ni kujiridhisha na kuona kama fedha za serikali zimetumika kikamilifu kama ilivyoelekezwa na serikali katika kuwaletea wananchi wake maendeleo kupitia miradi mbalimbali inatokelezwa na serikali ya awamu ya tano.
Waziri Jaffo alisema kuwa baada ya ukaguzi wa mradi wa barabara hizo ameipongeza serikali ya Mkoa wa Morogoro kwa kusimimamia kikamilifu hadi kukamilika kwa mradi huo .
Alitoa wito kwa viongozi na wananchi kwa ujumla kuhakikisha barabara hiyo inatunzwa miundombinu yake ikiwemo kulinda taa za nishati ya jua zilizowekwa barabarani ili kuweza kuifanya kuwa endelevu kwani kumekuwepo na baadhi ya maeneo barababara zinapowekwa miundombinu yake inaharibiwa na baaadhi ya watu wasio waadilifu na hivyo kuisabababishia serikali hasara.
‘’Ni lazima muhakikishe miundombinu ya barabara ,taa,na mitaro iliyojengwa inalindwa isiharibike ‘’alisema Waziri Jaffo.
Awali akisoma taarifa ya Mradi ,Mratibu wa Mradi huo Injinia Godwin Mpinzile alisema kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro ni miongoni mwa Halmashauri 18 zinazotekeleza mradi wa uboreshaji miji(ULGSP) kwa kutumia fedha za mkopo toka benki ya dunia.
Injinia Mpinzile alisema kuwa mradi huo ulioanza rasmi mwaka 2017ambao umegharimu kiasi cha shil Bil 12.6 kazi mbalimbali zimeweza kufanyika ikiwemeo kujenga njia za chini ya ardhi,kujenga makalvati,kuweka taa za barabarani .
‘’Pia kazi nyingine iliyofanyika ni pamoja na kuweka vivuko vya kuvusha magari ,kujenga vivuko vya waenda kwa miguu na pia kufanya ukamilishaji wa kazi ikiwemo kuweka alama ,matuta na kuchora mistari.
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt Kebwe Steven Kebwe alisema kuwa uongozi wa mkoa umekuwa ukifuatilia kwa ukaribu ujenzi wa mradi huo ili kuhakikisha fedha za serikali hazipotei na zinaendena na thamani halisi ya mradi.
Hata hivyo katika ukaguzi wa mradi huo wa barabara pia Waziri Jafo aliweza pia kukagua mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya uliopo katika Kata Kihonda Manispaa ya Morogoro ambapo aliahidi kuzifuatilia kiasi cha sh Mil 400 zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya mradi huo ambapo hadi hivi sasa hazijafika.
‘’Nimekuja kukagua kuona fedha zilizotumwa na serikali kama zimetekeleza vipi huu mradi lakini mmesema hamjaingiziwa hivyo nitafanya ufutailiaji ili fedha hizo niweze kujua zimekwama wapi , ili muweze kuzipata ili kukamilisha rasmi mradi huu’’alisema Waziri Jaffo.
Hata hivyo Mganga Mkuu wa Manispaa Baraka Jonas alisema kuwa lengo la mradi ni kujenga hospitali ya wilaya ya Manispaa itakayosaidia kuweka mfumo mzuri wa rufaa kuanzia zahanati kwenda kituo cha afya na hivyo kupunguza msongamano wa wagonjwa katika Hospitali ya rufaa ya Mkoa.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa