Waziri wa TAMISEMI Selemani Jaffo ameupongeza uongozi wa Manispaa ya Morogoro kwa matumizi mazuri ya fedha kiasi cha Tsh Bilioni 1,042,554,532.8 zilizoletwa na Serikali kuu kwaajili ya ukarabati wa majengo ya shule ya O-level na A-level katika shule ya Sekondari Morogoro.
Jaffo ameyasema ayo wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ukarabati wa shule hiyo unaofanywa kwa kutumia false Account na kusimamiwa na Mhandisi wa Manispaa ya Morogoro.
Akitoa taarifa ya ukarabati wa shule hiyo kaimu Mhandisi wa Manispaa Juma Gwisu ameeleza kuwa shule hiyo ni miongoni mwa shule 17 kongwe zilizobahatika kupewa fedha na Serikali kwa awamu ya pili kwaajili ya ukarabati.
Alieleza kuwa ukarabati wa shule hiyo ulianza tarehe 13/6/2019 na majengo yanayokarabatiwa ni mabweni tisa,nyumba za walimu 11,madarasa 27 na ujenzi wa madarasa mapya mawili,bwalo la chakula,jiko,maabara tatu,majengo ya utawala mawili,ofisi za walimu na vyoo.
Akizungumza mara baada ya kukagua maendeleo ya ukarabati wa shule hiyo Waziri Jaffo amepongeza ukarabati wa nyumba za walimu na kueleza baada ya ujenzi huo kukamilika walimu wataishi katika nyumba zilizo katika ubora.
Aidha amewasisitiza wanafunzi wa shule hiyo kusoma kwa bidii na kuona Serikali jinsi gani inavyowajari kwa kuwaboreshea mazingira ya kusomea.
"Mitihani inayofuata sitaki kuona kuna Division O katika shule hii,anzisheni kampeni ya kuondoa Division O na 4,na kila mwanafunzi amsaidie mwenzake katika kusoma ili nyote mpate ufaulu unaoridhisha"alisema Jaffo.
Pia Waziri Jaffo amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro kufuata taratibu na kumpandisha cheo Kaimu Mhandisi wa Manispaa kwa kuwa anafanya kazi nzuri katika usimamizi wa miradi ya maendeleo.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa