ZAHANATI mpya sita (6) ,Manispaa ya Morogoro zimeanza kutoa huduma huku baadhi ya huduma nyingine zikiwa mbioni kuanza kutolewa huku Manispaa ikianza na watumishi 18 katika zahanati zote 6 wakiwamo wauguzi 12,Madaktari wasaidizi 2 na Tabibu 2 ikiwa ni asilimia 20 ya mahitaji ya watumishi 15 kwa kila Zahanati.
Hayo yamezungumzwa na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Michael Waluse, katika ziara ya Menejimenti ya Manispaa ya kukagua miradi ya Zahanati hizo leo Aprili 01/2022.
Akizungumza katika ziara hiyo, amesema kuwa ndani ya siku 7-10 watahakikisha huduma zote muhimu zinazotakiwa kutolewa katika Zahanati hizo zinapatikana.
Waluse ,amesema katika ukamilishaji wa miradi hiyo ya ujenzi wa Zahanati 6, jumla ya shilingi 475,432,391.50/= zimetumika ambapo Milioni 379,554,891.50 sawa na silimia 75 ni mapato ya ndani na asilimia 21 kutoka Serikali kuu.
Kuhusu upatikanaji wa vifaa tiba,amesema , baadhi ya vifaa vimepatikana kwa kushirikiana na Ofisi ya Mganga Mkuu wa Manispaa na baadhi ya vituo vya kutolea huduma za afya 13 ambavyo vimechangia upatikanaji wa meza 32 zenye gharama ya Shilingi milioni 2,6000,000/=.
Aidha, , hadi sasa jumla ya vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi Milioni 11,051,496/= zimepelekwa katika kituo 1, ikiwa ni 13% ya mahitaji yote yanayohitajika katika vituo vyote 6 na hivyo kuwa na upungufu asilimia 87.
Pia, amesema ,juhudi zinazofanyika ili kukabiliana na upungufu huo, vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi milioni 36,970,540.88/= vimeagizwa bohari ya dawa (MSD) ikiwamo Hb Machine 6, Cuvette Hb 1000, BP Machine 6, Stethoscope 12, Bed Sheet 30, Matress 25, Digital BP Machine 6 na Digital thermometer 20.
Kwa upande wa Mganga Mkuu wa Manispaa ya Morogoro, Charles Mkombachepa, amesema juhudi mbalimbali zinafanyika ili kuhakikisha vituo hivyo, vinapata dawa kwa kuwa bado havina akaunti MSD.
Mkumbachepa, amesema baadhi ya vituo vya kutolea huduma vimechangia upatikanaji wa dawa zenye thamani ya Shilingi Milioni 3,261,300/= sawa na asilimia 3 ya mahitaji katika vituo hivyo 6 na hivyo kuwa na upungufu wa asilimia 97, na dawa zote zimepelekwa katika Zahanati ya Tungi.
Miongoni mwa Zahanati hizo ni Mgaza Kata ya Mindu, Sulatan Area, Mbuyuni, Tungi, Kihonda Maghorofani, na Kiwanja cha Ndege.
Mbali na Zahanti hizo, ziara hiyo imepata nafasi ya kukagua ujenzi wa Kituo cha Afya cha Lukobe kilichotengewa Milioni 250, ujenzi umeanza na unaendelea kwa kasi.
Mwisho, wajumbe wa CMT, wamewapongeza Baraza la Madiwani ,Madiwani wa Kata zenye Zahanti hizo, Viongozi wa Chama Cha CCM pamoja na Watendaji kwa kazi nzuri ya kusimamia vyema miradi hiyo inayolenga kutoa huduma kwa wananchi.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa