MSIMAMIZI wa Uchaguzi Manispaa ya Morogoro, Ndg. Waziri Kombo, ametangaza matokeo ya uchaguzi Serikali za Mitaa uliofanyika Novemba 24, ambapo katika matokeo hayo Chama Cha Mapinduzi CCM kimeibuka na ushindi wa wenyeviti wa mitaa kwa jumla ya mitaa 294.
Akizungumza na Waandishi wa habari Msimamizi wa Uchaguzi Kombo amesema jumla ya nafasi 148 za Wenyeviti wa Serikali za Mitaa wagombea wa CCM walipita bila kupingwa kwakuwa hakukuwa na mgombea wa chama kingine,Mitaa 146 vyama mbalimbali vilichukua fomu za kugombea ila wengine walijiondoa na wengine waliondolewa kwa kukosa vigezo.
Kombo ameeleza kuwa jumla ya Kata 9 na Mitaa 27 ndiyo iliyoshiriki uchaguzi huo baada ya kupita kwa michakato mbalimbali, na kukitangaza chama cha Mapinduzi (CCM) kufanikiwa kuibuka mshindi kwa kunyakua kura zote.
Aidha, amesema kuwa, awali walikuwa na Wagombea 17 wa vyama vya upinzani hivyo walipungua baada ya Viongozi wao wa juu kutoa tamko la kujiengua katika uchaguzi huo na kubakia wagombea wawili kwa upande wa nafasi za Wagombea wa wenyeviti wa Serikali za Mitaa.
Ndg. Waziri akitoa takwimu za matokeo hayo ameeleza kuwa kwa nafasi ya wenyeviti wa mitaa kata ya Uwanja wa Taifa uchaguzi ulifanyika katika mtaa wa Unguu ambapo jumla ya wananchi waliojiandikisha ni 287,idadi ya kura zilizopigwa na vyama vya siasa CCM kura 190,UDP kura 39 na kura moja imeharibika na hii kukifanya chama cha CCM kushinda kwa asilimia 80.Aidha kata ya Mindu uchaguzi umefanyika mtaa wa Kasanga ambapo idadi ya waliojiandikisha kupiga kura ni 789,idad ya kura zilizopigwa na vyama vya siasa CCM kura 448,CHADEMA kura 81,kura tatu zimeharibika na hii imekifanya chama cha CCM kushinda kwa asilimia 67.
'' Uchaguzi umemalizika kwa amani, matokeo kama mlivyo yasikia, chama cha CCM kimeweza kuibuka mshindi na kufanikiwa kuchukua mitaa yote, lakini awali tulikuwa na wagombea wengi wa Vyama vya Upinzani baadae wengine waliondolewa kwa kutokuzingatia kanuni na sheria na wengine walijiengua baada ya matamko ya viongozi wa vyama vyao ''. Amesema Kombo
Amesema kwa upande wa Wagombea nafasi za Wajumbe Mchanganyiko kulikuwa na nafasi za wagombea 882 na upande wa Wagombea Viti Maalumu Wanawake nafasi zilikuwa 588 katika Kata zote na nafasi ya wenyeviti wa mitaa nafasi zilikuwa 2kwa Mitaa yote ambayo uchaguzi umefanyika.
Miongoni mwa Vyama vilivyoshiriki katika uchaguzi huo ni pamoja na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), United Democreatic Party (UDP),Chama cha Mapinduzi(CCM) na Civic United Front(CUF).
Aidha, amewapongeza Wananchi waliojitokeza katika uchaguzi huo na kufanikisha uchaguzi kumalizika kwa amanai pasipo na uvunjifu wowote wa sheria.
Pia amewapongeza sana Wasimamizi wa uchaguzi kwa kusimamia vyema uchaguzi huo kwa kufuata misingi ya haki, huku akitoa rai kwa Viongozi waliochaguliwa waende kuwatendea haki wananachi wao kwa mustakabadhi wa maendeleo ya Taifa na Wananchi wao .
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa