MWENGE wa Uhuru Kitaifa 2025 umezindua miradi ya maendeleo Manispaa ya Morogoro yenye thamani zaidi ya bilioni 1.8 ,ambapo miradi yote imekubaliwa na Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa ,Ndg. Ismail Ali Ussi.
Mwenge huo wa Uhuru Kitaifa mwaka 2025,umekimbizwa Aprili 12-2025 kwa umbali wa Kilometa 91.4 na jumla ya miradi 09 imetembelewa na mwenge huo ambapo miradi 5 imezinduliwa, miradi 3 imeonwa na mradi 1 umetembelewa.
Akizungumza mara baaada ya kukamilika kwa ziara ya kuzindua miradi hiyo ya Mwenge, Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, amempongeza Mh. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuiletea Manispaa ya Morogoro miradi itakayokwenda kutatua kero za wananchi pamoja na kutoa huduma bora.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Emmanuel Mkongo, amesema miradi hiyo yenye thamani ya shilingi 1,827,898,119.12 , shilingi 542,341,811.45 fedha kutoka Serikali Kuu na shilingi 172,000,000.00 fedha kutoka Mapato ya ndani ya Manispaa, shilingi 130,000,000.00 ni fedha kutoka michango ya wananchi ,shilingi 983,556,307.67 ni michango ya wahisani na Mchango wa Mwenge wa Uhuru ni shilingi 39,600,000.00.
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini, Mhe. Abdulaaziz Abood, amesema ataendelea kuhakikisha anazidi kuisemea Manispaa ya Morogoro ili kufikiriwa zaidi katika miradi ya Maendeleo na kutumia nyenzo zake kusaidia maendeleo ili Manispaa ya Morogoro ifikishe adhima yake ya kuwa Jiji.
Naye Meya Manispaa ya Morogoro ,Mhe. Pascal Kihanga, amewashukuru Wananchi wote waliojitokeza katika mapokezi ya Mwenge na kuwataka kuendelea kuwa na imani na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Baraza la Madiwani la Manispaa ya Morogoro.
Miongoni mwa miradi iliyotembelewa na Mwenge ni Ujenzi wa Jengo la Utawala Kola Hill, uliogharimu shilingi 137,000,000.00, Mradi wa kuinua hadhi ya barabara ya Nongeni yenye kilometa 0.72 kwa kiwango cha zege uliotumia shilingi 478,299,123.20, mradi wa nishati safi na salama ya kupikia shule ya Sekondari Morogoro chini ya ufadhili wa EWURA , mradi wa ukarabati jengo la wagonjwa wa nje na ofisi za Utawala, Hospitali ya Mkoa Morogoro kwa gharama ya shilingi 505,257,184.67 kwa ufadhili kutoka Global Fund, mradi wa ujenzi nyumba ya watumishi 2 kwa 1 shule ya Sekondari Konga Mzinga kupitia mradi wa kuimarisha elimu ya Sekondari ( SEQUIP) wenye thamani ya shilingi 95,000,000.00, mradi wa kikundi cha Vijana cha uzalishaji wa mashine mbalimbali ( Hammer Metal Works Group) wenye thamani ya shilingi 35,000,000.00 kupitia mkopoa wa asilimia 10 ya Halmashauri , mradi wa viwanda vidogo vya kutengenezea vipuri (DEBU NG'IMBA FABRICATION WORKS) wenye thamani ya shilingi 70,000,000.00, mradi wa kutengeneza gundi za maji (Vibrant Chemical Company ltd wenye thamani ya shilingi 60,000,000.00, Makao ya Agape ya kulelea watoto wanaoishi mazingira hatarishi na watoto waliofanyiwa ukatili kwa kuwapatia malezi ya familia, na mradi wa ujenzi wa birika la maji lenye ujazo wa lita milioni 1 Mtaa wa nguvu kazi Kata ya Kihonda wenye thamani ya shilingi 61,126,074.55
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa