KAMATI ya Kudhibiti UKIMWI Manispaa ya Morogoro , imeitaka jamii kuongeza kasi ya mapambano ya vita dhidi ya maradhi hayo na kupunguza maambukizi kwa jamii kwa kupinga vitendo vya usagaji na ushoga hasa kwa wanafunzi na watoto.
Kauli hiyo imetolewa Aprili 17-2025 katika kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika Ofisi ya Kata ya Magadu kwa ajili ya kujadili shughuli mbalimbali zilizotekelezwa kwa kipindi cha robo tatu ya mwaka wa fedha 2025.
Aidha, Mhe. Chomoka,ameitaka jamii kuhakikisha ina kuboresha malezi ya watoto kwa kukemea vitendo vya usagaji na ushoga na ukatili unaofanywa kwa wanafunzi na watoto.
"Hakuna Taifa madhubuti la kesho kama hakuna malezi bora ya watoto, tunaiomba jamii iwe sehemu ya walimu, jamii iwe sehemu ya wachunga, jamii iwe sehemu ya malezi hawa ni watoto wetu wakiharibika tunahiaribu jamii ya kesho, maana miongoni mwao ndtio tunatarajia tutapata viongozi, miongoni mwao tunategemea tutapata watumishi, Mashekhe, tutapata mapadre, tutawapata watu wa kila aina ambao leo hii wapo kwenye jamii wanatuongoza”Amesema Chomoka.
Chomoka,amezitaka shughuli zote zinazoadhimishwa ndani ya Manispaa ziweke utaratibu wa watu kupima ili kubaini hali ya maambukizi ya UKIMWI.
Kwa upande wake mjumbe wa kamati hiyo, Mh. Amina Ziuye, amesema jamii ni lazima ichukue hatua zamaksudi kutoa elimu kwa wanafunzi wa shule za sekondari na msingi kwa kuwa wao ni wahanga wa kwanza wa vitendo hivyo.
Mh.Ziuye, ameongeza kuwa wapo baadhi ya vijana waliopo shuleni wameibua tabia ya kutaka kufanya mapenzi ya jinsia moja na watu wanaobainika au kuhisiwa kuwa na tabia hizo ambao baadhi yao tayari wamesha athirika na virusi vya UKIMWI.
Naye Mjumbe anayewakilisha mashirika binafsi kutoka Taasisi ya kusaidia masuala ya kisheria Morogoro Paralegal Centre, Chediel Senzighe, ameiomba kamati hiyo wataalam wa Afya kuwafikia walemavu kuwapa elimu ya kujikinga na maambukizi kwa kuwa kundi hilo halizingatiwi lakini maambukizi hayachagui kundi fulani la watu.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa