MKUU wa Wiala ya Morogoro, Mhe. Bakari Msulwa, amemuagiza Mhandisi wa Manispaa ya Morogoro kuongeza kasi katika kukamilisha Ujenzi wa Mkaburi ya waliofariki kwa ajali ya Moto Msamvu.
Kauli hiyo ameitoa leo Julai 7, 2020 wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujezni huo ikiwa yamebakia majuma machache katika kuadhimisha kumbukizi za wahanga hao.
Akizungumza na Waandishi wa habari, amesema kasi bado ni ndogo hivyo ametoa wiki moja ili hatua ya ujenzi iweze kufikia pazuri.
“Mhandisi na watu wako ongezeni kasi ya ujenzi, baada ya wiki moja nakuja hapa kupata mpango kazi na nikute kuna mabadiliko makubwa, vinginevyo hatutakubaliana kabisa na hii kasi mnayokwenda nayo, endeleeni na akazi kwani kazi inaonekana lakini kasi yake ni ndogo, “ Amesema DC Msulwa.
Aidha, amesema wamepewa dhamana ya kufanya kazi wafanye kazi milioni 18 zilizotolewa na Serikali ni kodi za wananchi hivyo wazitumie kwa ufanisi kazi ionekane na ikamilike kwa wakati na kwa viwango vilivyokusudiwa.
“’Hawa wenzetu wametangulia mbele za haki, Serikali na Wananchi imewapa heshima kubwa , na sisi tunawaombea kwa Mwenyezi Mungu awape kila aina ya msamaha, , nataka mpango kazi uwe mzuri tunachotaka ifikapo tarehe 1, Agosti ,2020 kila kitu kiwe kimekamilika kwa ajili ya madhimisho y ndugu zetu waliotangulia mbele za haki” Ameongeza DC Msulwa.
Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba, amemuagiza Mhandisi wa Manispaa ya Morogoro, Juma Gwisu kwenda na kasi zaidi ya kukamilisha ujenzi wa Makaburi hayo pamoja na mnara.
“Huu ni utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu , Mhe. Kassim Majaliwa, alivyokuja Manispaa yetu kutembelea makaburi kwa mara ya kwanza ambapo aliagiza tuboreshe na tuanze ujenzi wa makaburi pamoja na mnara mkubwa ambao utakuwa na majina yote ya marehemu kama moja ya njia za kuwaenzi, uzio tayari tumemaliza kujenga, Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro , Eng. Emmanuel Kalobelo ameshatupatia fedha kupitia mfuko wa maafa zilizokusanywa kwa ajili ya marehemu hawa, kwahiyo ujenzi umeanza , kikubwa niwaombe ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu wazidishe maombi wanapokwenda katika nyumba za ibada" Amesema Lukuba.
Lukuba, amesema katika ujenzi huo , litatengwa eneo rasmi litakalo tumika kwa ajili kufanyia sala na maombi kwa marehemu wote .
“Licha ya kuboresha makaburi lakini kutokana na uzito wa eneno, tumeona tutenge eneo la kufanyia sala na maombi, eneo hili dini zote watakaa na kila mtu ataomba kwa mujibu wa taratibu za dini yake , nizidi kuwaomba ndugu wa marehemu tuwe wavumilivu katika kipindi hiki kigumu, kuondokewa na ndugu zetu kusitufanye turudi nyuma kikubwa ni kuwaombea na kuendelea kufanya kazi kwa ajili ya familia zetu na maendeleo yetu tunatambua marehemu wameacha watoto, familia na tegemezi lakini yote ni mipango ya Mungu kila mtu atapitia njia hiyo muda na wakati ambao Mwenyezi Mungu atamuhitaji” Ameongeza Lukuba.
Amesema kuwa mara baada ya ujenzi huo kukamilika , kutakuwa na utaratibu wa maadhimisho ya kuwakumbuka na kuwaombea marehemu wote kila mwezi wa 8, tarehe 10 ambapo ndipo tukio la ajali ya moto lilitokea.
Ikumbukwe kuwa, mkasa huo ulitokea majira ya saa mbili asubuhi ya Jumamosi baada ya lori lilibeba shehena ya petroli kuanguka katika mji wa Morogoro, na watu kuanza kuchota mafuta yaliyomwagika kisha mlipuko mkubwa kutokea.
Naye Mhandisi wa Manispaa ya Morogoro, Juma Gwisu, amesema ujenzi wote wa makaburi, fensi pamoja na mnara utagharimu kiasi cha shilingi Milioni 35, ambapo mpaka sasa wameshaingiziwa Shilingi Milioni 18 na mradi huo unatarajiwa kumalizika Julai 26, 2020.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa