Kamati ya Fedha na Utawala ya Manispaa ya Morogoro imeipongeza Menejimenti ya Manispaa hiyo kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa katika Kata mbalimbali za Manispaa.
Kamati imetoa pongezi hizo hivi karibuni Oktoba 2023 ilipokuwa katika ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa ndani ya Manispaa.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mheshimiwa Pascal Kihanga, ambaye pia alikuwa kwenye ziara hiyo, amemshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Daktari Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuipatia Manispaa ya Morogoro fedha za miradi ya maendeleo na kuongeza kuwa Baraza la Madiwani kupitia Kamati zake za Kudumu litaendelea kufanya kazi zake ipasavyo kuhakikisha kuwa miradi inatekelezwa kwa ubora uliuokusudiwa na thamani ya fedha katika miradi inaonekana.
MWISHO
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa