WAJUMBE wa Kamati ya Huduma za Uchumi ,Afya na Elimu Manispaa ya Morogoro , wamefanya ziara ya kukagua miradi ya Maendeleo huku wakionesha kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa miradi hiyo.
Ziara hiyo imefanyika tarehe 24/1/2025 na kutembelea Shule ya Sekondari ya ghorofa ya Boma B pamoja na Ujenzi wa Jengo la Utawala na ukarabati wa majengo Shule ya Msingi Mji Mkuu,
Wakizungumza kwa nyakati tofauti tofautii , wajumbe hao wamepongeza jitihada za serikali katika kihakikisha huduma zinawafikia wananchi wake kwani hatua ya miradi yote ipo hatua nzuri.
sambamba na hayo Wajumbe hao wameagiza Uongozi wa Manispaa kuhakikisha kwamba Shule ya Sekondari ya Ghorofa ya Boma B waalimu wanatoa ufaulu mzuri kulingana na ubora wa shule hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Kiwanja cha Ndege, Mhe. Majuto Mbuguyu, amewashukuru wajumbe kwa ziara hiyo huku akiwahahakikishia kusimama kidete kuona miradi hiyo inakamilika kwa wakati na kuanza kutoa huduma kwa wananchi.
Mhe. Mbuguyu amewapongeza Madiwani wa Kata ya Boma na Mji Mkuu pamoja na Uongozi wake wa Kata kwa kusimamia vyema miradi hiyo.
Naye, Diwani wa Kata ya Mji Mkuu, Mhe. Hassan Maringo, amesema miradi yote inaendelea vizuri na Uongozi wa Kata ya Mji Mkuu umekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wanasimamia vyema miradi hiyo.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Christopher Komba,amesema Manispaa kwa kushirikiana na Menejimenti watahakikisha miradi inatekelezwa kwa kasi na kuendelea kutoa huduma kwa wananchi.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa