ALIYEKUWA Naibu Meya Manispaa ya Morogoro, ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Sabasaba, Mhe. Mohamed Yahaya Lukwele,amepita tena kwa kishindo katika uchaguzi wa Unaibu uliofanyika katika Mkutano wa kawaida wa mwaka wa Baraza la Madiwani.
Uchaguzi huo umefanyika leo Julai 19/2022, katika Ukumbi wa Mikutano wa Kilakala Soko Kuu la Chifu Kingalu Morogoro.
Mhe. Lukwele, amepita kwa kishindo kufuatia wajumbe wa baraza 38 wote kumpitisha bila kupingwa mara baada ya kupata nafasi hiyo baada ya uchaguzi wa Chama chake cha CCM kumtangaza kuwa mshindi.
Akizungumza mara baada ya ushindi huo, Mhe. Lukwele, amewapongeza wajumbe wa Baraza kwa kumuamini tena kushika nafasi hiyo.
Aidha, amesema ili kufanikisha mipango yote ambayo Manispaa imepanga , umoja na mshikamano unahitajika katika kufikia maendeleo.
“ Niwapongeze sana wajumbe, mmefanya upendo, mmeniamini na kunipa ridhaa ya kuongoza tena kwa kiti hiki cha mwaka wa pili cha Unaibu Meya, niwaahidi ushirikiano ili Manispaa yetu iweze kupiga hatua” Amesema Mhe. Lukwele.
Naye Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro ,amewataka wajumbe wa Baraza kuendeleza ushirikiano ili utekelezaji wote wa mpango wa mwaka wa fedha 2022/2023 ufanyike kwa ufanisi .
“SENSA KWA MAENDELEO ,JIANDAE KUHESABIWA TAREHE 23/08/2022”
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa