Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, Pascal Kihanga amewaondoa hofu Madiwani na wananchi wa Manispaa kuhusu utekelezaji wa agizo la Rais Dk John Magufuli kwa uliokuwa Mfuko waLAPF kukabidhi stendi ya kisasa ya mabasi ya Msamvu chini ya umiliki wa Manispaa hiyo.
Alisema , agizo hilo na utekelezaji wake upopale pale na mchakato unatekelezwa chini ya Mamlaka mbalimbali za Serikali.
Meya Kihanga alitoa ufafanuzi huo wakati akijibuswali kutoka kwa Diwani wa Kata ya Sabasaba , Mudhihir Shooaliyetaka kujua lini kituo cha mabasi hicho kitamilikiwa na Manispaahiyo kwa asilimia 100 tofauti na ilivyokuwa kwa sasa ambapokituo kinamilikiwa kwa ubia wa Manispaa na LAPF.
Baraza hilo lilikutana Aprili 30, mwaka huu katika kikaochake cha kawaida cha robo ya tatu kwenye ukumbi wa Manispaa , ambapo katikajibu la msingi , Meya huyo ambaye ni mjumbe wa bodi ya kituo cha mabasi Msamvualisema kuwa, mchakato wa kukikabidhi kituo hicho kwa Manispaa yaMorogoro unaendelea.
Kihanga alisema , tayari Rais Magufuli aliagiza mamlakambalimbali kushughulikia jambo hilo na hivyo aliwataka madiwani, wananchi nawadau wengine kuwa wavumilivu kuwa muda muafaka ukifika watakabidhiwa stendi hiyo.
Naye Diwani wa viti maalumu ,Hadija Kibati kupitiakikao cha Baraza hilo ameiomba Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) kuwekautaratibu wa kuwafuata wananchi kwenye ofisi za kata ili waweze kutoa huduma nasio kujifungia ofisini.
Ombi la Diwani huyo ambalo liliungwa mkono nawajumbe wa bazara la madiwani ni baada ya Mkurugenzi wa Manispaa ,John Mgalula kutakiwa kutoa ufafanuzi kuhusu suala vitambulisho vya Taifaambavyo wananchi wanatakiwa kuvitumia kwenye zoezi la usajili wa laini za simukuanzia Mei 1 hadi Desemba 31 mwaka huu.
Diwani huyo alisema , kuwa kwa sasa ofisi za NIDA zilizopopembezoni mwa mji wa Morogoro, hivyo wananchi wamekuwawakitumia gharama kwenda kuulizia vitambulisho ama kupata ufafanuzi wowotekuhusu vitambulisho vyao huku wengine wakishindwa kumudu gharama hizo.
Alisema kuwa licha ya vitambulisho vyaTaifa kuwa muhimu , lakini bado idadi kubwa ya wananchi wa Manispaa ya Morogorohawajavipata hivyo aliiomba Nida kuharakisha zoezi la utoaji wa vitambulishohivyo ili kuepuka usumbufu.
Kutokana na hoja hiyo, Meya wa Manispaa yaMorogoro, Kihanga alisema kuwa, ni vema Nida ikawafuata wananchikwenye maeneo waliyopo kama walivyofanya wakati wa kuwaandikisha badala yawananchi kutembea umbali mrefu kufuata ama kuulizia vitambulisho hivyo.
Kwa upande wake diwani wa viti maalumu , DorothMwamsiku aliomba Halmashauri kuwapa kifuta jasho wenyeviti wa mitaa wanaotarajia kumaliza muda wao wa uongozi Oktoba mwakahuu kwa kuwa wamekuwa ni msaada mkubwa katika mambombalimbali ya maendeleo ya Manispaa .
Kufuatia swali hilo , Mkurugenzi wa Manispaa Mgalula alisema kuwa, mpaka sasa hakuna bajeti yoyote iliyotengwa kwa ajili ya kuwalipa kifutajasho wenyeviti wa mitaa japokuwaalikiri kwamba wenyeviti hao kuwa ni sehemu ya maendeleo ya Manispaa yaMorogoro.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa