HALMASHAURI ya Manispaa ya Morogoro imekiomba Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kilichopo chini ya Wizara ya Viwanda ,Biashara na Uwekezaji kushirikiana katika kutangaza maeneo yake ya ardhi ili yaweze kupata wawekezaji kwenye sekta ya viwanda na kilimo.
Ombi hilo limetolewa na Meya wa Manispaa Mhe. Pascal Kihanga alipotembelea banda la TIC kanda ya Mashariki katika viwania vya maonesho ya Nanenane vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kanda ya Mashariki mkoani Morogoro.
Kihanga alisema Manispaa ina eneo kubwa la uwekezaji na watu wenye nia ya kuwekeza katika sekta ya viwanda na kilimo wataoneshwa maeneo kwani ni maeneo mazuri kufanya uwezakaji huo .
“ Tunaomba tushirikane katika kutangaza maeneo yetu ya uwekezaji ,mwekezaji akija Manispaa ya Morogoro sisi tutamwonesha maeneo ya uwekezaji karibu na eneo la Nane Nane na tumeyapanga kuwa ni sehemu ya uwekezaji “ alisema Kihanga
Kwa upande wake Ofisa Uwekezaji mkuu wa TIC , Fidelis Obanga akijibu ombi la Meya wa Manispaa alisema kuwa watu wote watakaotembelea maonesho hayo hasa katika banda lao wanapewa taarifa za kuwepo eneo kubwa ya ardhi ndani ya Manispaa ya Morogoro kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda na kilimo.
“ Kwa sasa tumetembelewa na watu wengi kwenye banda letu lakini wawili wameonesha nia ya kutaka kuwekeza ambapo mmoja wao ni kwenye eneo la ujenzi wa kiwanda cha mbolea na endapo atarejea kutaka mrejesho tutamwarifu “ alisema Obanga.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa