HALMASHAURI ya Manispaa ya Morogoro imeweka mpango wa kuanza awamu ya kwanza ya ujenzi wa soko kuu jipya kwa kutumia fedha za Mfuko wa uboreshaji wa halmashauri na Miji (ULGSP) kwa gharama ya Sh bilioni 9.5 katika mwaka huu wa fedha, 2018/2019 .
Mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa Morogoro, John Mgalula alisema hayo wakati wa kikao malaumu cha bajeti cha baraza la madiwani wa halmashauri kilichokuwa kikiongozwa na Mstahiki Meya , Pascal Kihanga.
Mgalula aliwahakikishia madiwani akiwemo Daud Salum ambaye yeye na wenzake walihoji kuchelewa kuanza kwa ujenzi wa soko jipya la kisasa kwani walikuwa wanahitaji baadaye kuwafahamisha wananchi walivyotekeleza ilani ya uchanguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kabla ya kuingia kwenye uchaguzi mkuu wa 2020.
“ Nawahakikishia waheshimiwa madiwani kuwa ujenzi wa soko kuu jipya la kisasa , mchakato wake umefikia hatua nzuri na mwaka huu wa fedha ujenzi utaanza kwa awamu ya kwanza kwa kutumia fedha za Mfuko wa ULGSP kinachofanyika kwasasa ni taratibu za kutangaza zabuni kwa ajili ya ujenzi huu zinaendelea” alisema Mgalula.
Kwa upande wake , Meya wa Manispaa alisema , halmashauri katika mwaka wa fedha wa 2018/2019 mpango mkakati uliowekwa ni pamoja na kuboresha sekta ya afya kwa kukamilisha ujenzi wa kituo cha afya Sina, na Misongeni .
Pia alitaja uendelezaji na kuanzisha ujenzi wa zahanati za Mbuyuni, Sultani Area, Kibwe, Konga, Tungi , Kauzeni na Kiwanja cha Ndege , kuendeleza ujenzi wa hospitali ya wilaya na ujenzi wa chumba cha upasuaji katika kituo cha afya Mafiga lengo ni kusongeza huduma za afya karibu na jamii.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa