Tarehe 30.10.2023, Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini, Mheshimiwa Dkt. Abdulaazi Abood, amezuru shule za Sekondari Lukobe na Kingolwira na kutoa kompyuta sita kwa kila shule kwa ajili ya masomo ya TEHAMA.
Mheshimiwa Abood amesema, utoaji wa kompyuta hizo ni mwendelezo wa zoezi lake la kutoa kompyuta katika Shule za Sekondari za Manispaa ya Morogoro ili kusaidia katika masomo ya TEHAMA.
Naye Diwani wa Kata ya Lukobe, Mhe. Selestine Mbilinyi, amempongeza Mbunge Abood kwa kujali elimu hata kutoa vifaa hivyo ambavyo vitasaidia wanafunzi katika masomo yao na kufanya vizuri kitaaluma.
Aidha, walimu waliopokea vifaa hivyo kwa nyakati tofauti wamemshukuru Mheshimiwa Abood kwa kuwapatia vifaa hivyo ambavyo vitakuwa msaada mkubwa katika kuongeza ufanisi wa ufundishaji na ujifunzaji.
MWISHO
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa