• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Morogoro Municipal Council
Morogoro Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
    • Wakuu wa Divisheni na Watumishi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Divisheni
      • Rasilimaliwatu na Utawala
      • Miundombinu, Uendelezaji wa Vijijini na Mijini
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ugavi na Manunuzi
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Fedha na Uhasibu
      • Taka Ngumu na Usafishaji
      • Michezo, Sanaa na Utamaduni
      • TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Mazingira
    • Miundombinu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoisha
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Fomu ya Maombi
    • Waraka
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
  • Market
    • Market line 1
    • Maket line 2

MKURUGENZI MANISPAA YA MOROGORO ATOA WITO KWA JAMII NA WAZAZI KUONDOKANA NA MILA KANDAMIZI DHIDI YA WATOTO WAKIKE

Posted on: October 12th, 2020

MKURUGENZI wa Manispaa ya Morogoro, Sheilla Lukuba, ametoa wito kwa Jamii na Wazazi kuachana na mila na desturi zinazolenga kumkandamiza Mtoto wa kike.

Kauli hiyo ameitoa leo, Oktoba 12, 2020 , ikiwa imepita siku moja tangia Mtoto wa kike aadhimishe sikukuu hiyo ambapo hufanyika kila mwaka ifikapo Oktoba 11,2020.

Akizungumza na Waandishi wa habari, Lukuba, ameitaka Jamii na Wazazi kuacha mila na desturi ya kuwalazimisha watoto wa kike kuolewa wakiwa na umri mdogo na badala yake wapeleke watoto shule wakapate elimu ili waweze kutimiza ndoto zao.

“Inashangaza sana kuona bado mnazikumbatia mila na desturi kandamizi zinazo wanyanyasa Wanawake,kwani Wanawake pia wanayo nafasi na haki ya kupanga na kuamua mambo hivyo tuache kuwaamulia vitu wasivyovitaka, Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, imekuwa mstari wa mbele kuwaamini Wanawake hususani katika nyadhifa mbalimbali za kiutawala na Uongozi, hivyo lazima tuwape vipaumbele Watoto wa kike na kuwaondolea mila kandamizi ili wafikie malengo katika Ujenzi wa Taifa ”Amesema Lukuba.

Lukuba, amesema bado kuna kesi ambazo zinatokea za Watoto wa kike kulazimishwa kuingi katika mahusiano , hivyo katika hilo Manispaa yake hawatawafumbia macho watu wa namna hiyo, atahakikisha kwa kushirikiana na vyombo vya dola ili watu wanaoenda kinyume na haya wakamatwe na kuchukuliwa hatua kali kwani kitendo hicho kinatambulika kama ubakaji kwani vitendo hivyo wamekuwa wakifanyiwa mabinti wenye umri mdogo sana.

“Nasema hivi hatuwezi kuwafumbia macho watua ambao bado wanaendeleza mila na tamaduni ambazo hazina faida yeyote kwa jamii sio wa kuwachekea chekea nataka wote wakamatwe na kesi zao ziende mahakamani haraka ili tabia hii iweze kukoma na iwe fundisho, tunataka Jamii zenye uelewa dhidi ya Mtoto wa kike, kwahiyo tutahakikisha tunashirikiana vizuri na Wazazi ili haya yanayofanyika yasitokee, Ustawi wa Jamii upo naamini wanafanya kazi zao vizuri sana katika haya ya unyanyasaji, tukiona mtu hawezi kubadilika basi vipo vyombo ambavyo vitambadilisha kwa mujibu wa Sheria za nchi" Ameongeza Lukuba.

Aidha, amewataka Wazazi na jamii kuwekeza elimu kwa Watoto wao wa kike badala ya kuwa na imani za tofauti za kuwasomesha Watoto wa kiume pekee.

Pia ,amewataka Wazazi kukaa na Watoto wao kuwafundisha maadili mazuri na tabia njema kwani maadili mengi yanapotea kutokana na Wazazi wengi kusahau majukumu yao katika maadili ya Watoto wao.

Mwisho, amewaonya watu wenye mila potofu katika Manispaa ya Morogoro , na kusisitiza kuwa hilo halikubaliki kisheria na yeyote atakaebainika anaendelea na zoezi hilo hatosita kumchukulia hatua dhidi yake hivyo wanapaswa kufuata sheria na taratibu kwa kutenda haki kwa watoto wa kike.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI February 19, 2025
  • FURSA YA UWEKEZAJI KWA NJIA YA UBIA(PPP) February 18, 2025
  • ZABUNI YA UPANGISHAJI ENEO LA ROCK GARDEN MANISPAA YA MOROGORO August 16, 2022
  • MAPOKEZI YA HELA ZA OC KWA MWEZI JULAI 2022 KIASI CHA TSH 8,714,000.00 August 10, 2022
  • Angalia Yote

Habari Mpya

  • BARAZA LA MADIWANI NA WATUMISHI MANISPAA YA MOROGORO WAFANYA ZIARA YA MAFUNZO HALMASHAURI YA JIJI TANGA

    April 26, 2025
  • KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI MANISPAA YA MOROGORO YATAKA KASI VITA DHIDI YA MAAMBUKIZI MAPYA.

    April 17, 2025
  • KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI, AFYA NA ELIMU MANISPAA YA MOROGORO YARIDHISHWA NA KASI YA MIRADI YA MAENDELEO.

    April 15, 2025
  • MWENGE WA UHURU KITAIFA WAZINDUA MIRADI YA MAENDELEO YENYE THAMANI ZAIDI YA BILIONI 1.8.

    April 12, 2025
  • Angalia Yote

Video

MEYA KIHANGA AKABIDHI TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI ZAIDI YA 1600 WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Leseni za Biashara
  • Sheria Ndogo za Manispaa ya Morogoro
  • Sisi ni Nani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Tamisemi
  • Morogoro Modern Market system (outside)
  • Tovuti ya Utumishi
  • Morogoro Modern Market System (LAN Network)
  • Tovuti Rasmi ya Ikulu
  • Tovuti ya RAS Morogoro

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro

    Anuani: 166 morogoro

    Simu: 0232614727

    Simu: 0734-039300

    Baruapepe : info@morogoromc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa