• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Morogoro Municipal Council
Morogoro Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
    • Wakuu wa Divisheni na Watumishi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Divisheni
      • Rasilimaliwatu na Utawala
      • Miundombinu, Uendelezaji wa Vijijini na Mijini
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ugavi na Manunuzi
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Fedha na Uhasibu
      • Taka Ngumu na Usafishaji
      • Michezo, Sanaa na Utamaduni
      • TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Mazingira
    • Miundombinu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoisha
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Fomu ya Maombi
    • Waraka
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
  • Market
    • Market line 1
    • Maket line 2

MKUU WA WILAYA MOROGORO AWACHUKULIA HATUA KALI WANAFUNZI WALIOFANYA UHARIBIFU WA MAJENGO SHULE YA SEKONDARI MJI MPYA

Posted on: November 15th, 2019

MKUU wa Wilaya ya Morogoro , Mhe. Regina Chonjo, amemuagiza Mkuu wa Shule ya Sekondari Mji Mpya, Mwalimu Zakayo John,  kutotoa  vyeti vya kuhitimu kidato cha nne kwa  wanafunzi wote waliohusika na uharibifu wa mioundombinu katika shule hiyo.

Agizo hilo amelitoa leo Novemba 15, 2019, wakati akitembelea Shule hiyo ili  kuona maeneo ambayo wanafunzi walifanya uharibifu.

Akizungumza na Waandishi wa habari, amesema Wanafunzi waliofika na Wazazi wao wataadhibiwa kwa viboko mbele ya wazazi wao  na kupewa adhabu ndogo ndogo lakini wale waliokaidi wito hawatapa vyeti vya kuhitimu elimu yao ya kidato cha nne.

Aidha , amewataka wanafunzi wote  kuacha uharibu wa miundombinu badala yake wafanye kile kilichowapeleka ili kukwepa adhabu na kuchukuliwa hatua za kinidhamu.

" Wanafunzi hamjambo? natumaini mmefurahia mazingira haya tofauti na yale mliyokuwa nayo, lakini ni kwanini mnashindwa kuyatunza? mmeanza kuharibu miundombinu ya shule na kuiba taa za shule,  Serikali imejenga Shule hii ili msome na mpate elimu bora kwa maendeleo yenu,  sasa hawa wenzenu walikosa aibu na nidhamu kwa uharibifu huu nataka waadhibiwe na viboko mbele ya wazazi wao na kupewa adhabu za kupanda miti , wale wa kidato cha nne waliohusika nawapa siku saba kuanzia leo waripoti shuleni wamwagilie miti wasipofanya hivyo nawao tunawafungia matokeo yao na kuwanyima vyeti na wale wa kidato cha tatu wakati wa likizo asubuhi mfike na muhakikishe miti yote ina mwagiliwa na asikose mtu" Amesema DC Chonjo.

Amesema Shule hiyo haijafunguliwa rasmi na imejengwa kwa thamani kubwa ya fedha takribani Bilioni 1 na Milioni 400 zimetumika katika ujenzi huo  , hivyo katika kuwasaidia wanafunzi wasome waliona ni vyema wakamuomba   Waziri wa TAMISEMI, Mhe. Selemani Jaffo, ili kuitumia lakini cha kushangaza wanafunzi wapuuzi wameanza kuonesha tabia chafu.

"'Nipende kuwaeleza Wanafunzi sisi tunawapenda sana, tumeamua Shule hii  iwe miongoni mwa shule zitakazo toa masomo ya ngazi ya juu ya elimu ya Sekondari A. Level, lakini mmeanza kuharibu miundombinu je tutafika kweli? nilitarajia siku moja  mnipatie ugeni rasmi katika Mahafali yenu lakini kwa hatua hii kwakweli mnanitia mashaka, sasa nafasi mliyonayo muitumie vizuri, kwani uchumi wa Viwanda unategemea  Taifa lenye Elimu"" Amesisitizia DC Chonjo.

Amesema hakutakuwa na Viwanda kama hakuna wataalamu wenye uelewa wa kutosha wa kuendesha Viwanda, hivyo amewataka Wanafunzi wajirekebishe na kujenga tabia njema kwani hategemei kurudi katika Shule hiyo kwa kosa hilo.

 Naye, Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga, amewaomba Wanafunzi wabadilike na kuachana na tabia mbaya ya kuharibu miundombinu ya Shule.Amewataka Wanafunzi wanapokwenda Shule , wawe na wazo moja la kusoma na si vinginevyo.

Katika hatua nyengine, Mstahiki Meya , Mhe. Pascal Kihanga, amemuomba Mkurugenzi wa Manispaa ya Halmashauri ya Morogoro, kuwapatia Shule hiyo jumla ya miche 300 ya miti kwa ajili ya kuboresha mazingira katika Shule hiyo.

"' Mkurugenzi nikuombe pale Manispaa tuna bustani ya miche, wapatie Shule hii miche 300 kwa kuanzia na jua kuna Wanafunzi ambao vichwa vyao ni vibaya watang'oa, , kwakuwa wamesema hawana bajeti ya kununua miche, tuanze na hiyo ili tuipendezeshe shule hii kwani mazingira yaliyopo kwa sasa hayaendani na ubora wa shule ilivyo" Amesema Mhe. Kihanga

Katika kuona miti hiyo inastawi, amemtaka Mkuu wa Shule kuhakikisha mara baada ya kupokea miche hiyo, wahakikishe  kila mwanafunzi anapatiwa  mti wake kwa ajili ya kuumwagilia asubuhi na jioni kabla ya kurudi  nyumbani.

Kwa upande wa Diwani wa Kata ya Mji Mpya, Mhe. Wenseslaus Kalogeries, amewataka Wanafunzi hao kulinda miundombinu ya shule na kila mmoja awe mwangalizi wa mwenzake na endapo kuna mwanafunzi amefanya uharibu atoe taarifa kwa mwalimu.

Amesema watakutana na Bodi ya Shule ili kuhakikisha matukio kama hayo hayatokei tena katika Shule hiyo na kumtaka Mkuu wa Shule kuwasilisha taarifa za wanafunzi watukutu wote kwenye bodi ya shule ili wachukuliwe hatua za kisheria.

 

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI February 19, 2025
  • FURSA YA UWEKEZAJI KWA NJIA YA UBIA(PPP) February 18, 2025
  • ZABUNI YA UPANGISHAJI ENEO LA ROCK GARDEN MANISPAA YA MOROGORO August 16, 2022
  • MAPOKEZI YA HELA ZA OC KWA MWEZI JULAI 2022 KIASI CHA TSH 8,714,000.00 August 10, 2022
  • Angalia Yote

Habari Mpya

  • BARAZA LA MADIWANI NA WATUMISHI MANISPAA YA MOROGORO WAFANYA ZIARA YA MAFUNZO HALMASHAURI YA JIJI TANGA

    April 26, 2025
  • KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI MANISPAA YA MOROGORO YATAKA KASI VITA DHIDI YA MAAMBUKIZI MAPYA.

    April 17, 2025
  • KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI, AFYA NA ELIMU MANISPAA YA MOROGORO YARIDHISHWA NA KASI YA MIRADI YA MAENDELEO.

    April 15, 2025
  • MWENGE WA UHURU KITAIFA WAZINDUA MIRADI YA MAENDELEO YENYE THAMANI ZAIDI YA BILIONI 1.8.

    April 12, 2025
  • Angalia Yote

Video

MEYA KIHANGA AKABIDHI TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI ZAIDI YA 1600 WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Leseni za Biashara
  • Sheria Ndogo za Manispaa ya Morogoro
  • Sisi ni Nani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Tamisemi
  • Morogoro Modern Market system (outside)
  • Tovuti ya Utumishi
  • Morogoro Modern Market System (LAN Network)
  • Tovuti Rasmi ya Ikulu
  • Tovuti ya RAS Morogoro

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro

    Anuani: 166 morogoro

    Simu: 0232614727

    Simu: 0734-039300

    Baruapepe : info@morogoromc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa