MSTAHIKI Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga, amemtaka mkandarasi wa ujenzi wa mradi wa Stendi Mpya ya Daladala, unaosimamiwa na Mhandisi Mshauri M/s HOWARD HUMPHREYS TANZANIA LTD, kuhakikisha mradi huo unakwenda kwa mkasi kubwa.
Hayo ameyasema leo, Novemba 14, 2019 mbele ya waandishi wa habari, mara baada ya Kamati ya fedha na Uongozi kufanya ziara ya kutembelea mradi huo.
Akizungumza na waandishi wa habari, Meya Kihanga, amesema hajaridhishwa na kasi ya ujenzi huo unaoendela kwa sasa, hivyo amemtaka mkanadarasi kufanya kazi uskiu na mchana kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa muda uliopangwa.
Amesema lengo la kutekeleza mradi huo wa Stendi ya Daladala unaogharimu Shilingi Bilioni 4.1 ndani ya Manispaa ya Morogoro , umetokana na hali halisi ya Stendi iliyopo katikati ya Mji kuzidiwa na wingi wa watu, wingi wa magari na ukuaji wa mji.
" Mkandarasi huu mradi upo chini ya utekelezaji, kama kuna mahala mnakwama mtuambie, haiwezekanai kila tukija hapa hatuoni matokeo, tunataka mradi ukamilike, hizi pesa tunazotumia ni za watu na ifikapo mwezi wa Disemba, tarehe 31, 2109 pesa hizi zinachukuliwa na wenyewe, nadhani mnajua hali tuliyokuwa nayo Manispaa, tujitahdi ili hizi pesa zisiondoke, fanyeni kazi kwa spidi kubwa na pale mnapoona mnakwama mtushirikishe kwa haraka tuone namna gani tunaweza kusaidiana ili ujenzi huu ukamilike na ulete tija kwa wananchi na kutoa huduma bora" Amesema Meya Kihanga.
Naye Msimamizi wa Miradi ya Benki kuu ya Dunia, Eng. Mnene James , amesema ujenzi huo unasua sua kutokana na mvua zilizonyesha hivi karibuni, hivyo wataongeza kasi ya ujenzi ili kukamilisha mradi huo kwa wakati.
Amesema ujenzi huo unajumuisha Jengo la Utawala, jengo la huduma, Maeneo ya Maegesho pamoja na eneo la maegesho ya Daladala.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa