Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Stephen Kebweamewatoa hofu wananchi wa Kata ya Mindu wanaoishi karibu na Bwawa laMindu kwa kuwataka wawe watulivu wakisubiri maelekezo kutoka Serikalini kuhusuchangamoto inayojitokeza katika eneo wanaloishi.
Mkuu wa Mkoa ametoa kaulihiyo Februari 20, 2019 wakati akizungumza na wananchi wamitaa mitatu ya Kata ya Mindu wanaokaa karibu na Bwawa hilo .
Lengo la mkutano huo ulikuwani kuwafikishia ujumbe ,Mawaziri wanane waliotembeleaBwawa hilo hivi karibuni na kuangalia changamoto ya sheria ya mita 60 na mita500 kwa wakazi na shughuli za kibinadamu zinazoendeshwa jirani na bwawa hilo.
Katika ziara hiyo ambapo wakaziwengi walionekana kupatwa na mshtuko wakidhani Mkuu huyo wa Mkoa amepelekaujumbe tofauti na ule uliotolewa na timu ya Mawaziri wananewaliofika katika bwawa hilo hivi karibuni.
Hata hivyo Mkuu waMkoa wa Morogoro aliwatoa hofu akisema kuwa yeye hana jambo jinginejipya zaidi la ujumbe wa Mawaziri hao.
“Kwa hiyo tumeona tuje tuwatoe hofuwananchi kuhusu hili wala hakuna jambo jingine lolote lile” alisema Dkt. Kebwe
Mkuu wa mkoa pia aliwatahadharishawananchi hao kutojimilikisha maeneo katika eneo hilo wala kudanganywa na mtu auwatu kwa kuuziwa viwanja katika eneo hilo ambalo maamuzi yake yanasubiriwakutolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli.
“Hili liko mikononi mwa Mwenyenchi, asije akatokea mtu akawaambia jamani hapa kuna kipande cha shilingi lakimoja au shilingi laki mbili, tujihadhari kwa hilo” aliongeza Dkt. Kebwe .
Nao baadhi ya wananchi wanaoishimitaa mitatu katika Kata yaMindu iliyopo ndani ya mita 500, Bi RayaSubaha, bi Nuru Salum na Andrea Kalinga kwanyakati tofauti walitoa shukrani zao kwa mkuu wa mkoa waMorogoro kufika eneo hilo na kuwasilisha maelezo ya Mawaziri hayo yakuwaondoa hofu juu ya kuvunjiwa nyumba zao huku wakisubiri huruma zaRais Dk John Magufuli.
“ Mimi nimeishi eneohili tangu bwawa hili linajengwa hadi sasa , sina pakwenda na umri wangu nimkubwa , tunamwomba mheshimiwa Rais atuangalie sisi wananchi wanyonge “alisema Mzee Rashid Lugendo.
Awali, kamati ya Mawaziri wananeiliyoundwa na Rais ikiongozwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba naMaendeleo ya Makazi, William Lukuvi ilitembelea Bwawa hilo na ikatoamaelekezo kwa mkoa huo kusimamisha mipango yoyote inayoendeleakatika eneo hilo ukiwemo wa kutaka kuwahamisha wakazi wa eneo hilo hadi hapowatakapopewa maelekezo kutoka Serikalini.
Kamati ya mawaziri haoimepewa jukumu kufuatilia maeneo yote ya hifadhi yanayodaiwakuvamiwa na wananchi katika maeneo mbalimbali nchini, na ikiwepo eneo la Bwawahilo kwa niaba ya kamati hiyo pia ilizuia watu wasiendelee kuongezeka katikaeneo hilo.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa