Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Martine Shigela, amegawa jumla ya hekari 4500 kwa wakazi wa Kiegea Manispaa ya Morogoro kufutia kutatauliwa mgogoro uliokuwa ukiwakabili baina yao pamoja na Mmiliki wa eneo hilo la Star City.
Hatua hiyo ya ugawaji wa hekari 4500 na kutatua mgogoro huo kwa wananchi, imefanyika Juni 18/2021 katika eneo la shamba hilo la Star City lililopo Kiegea Manispaa ya Morogoro.
Akizungumza na wananchi hao wakati wa mkutano wa hadhara wa kuongea na wananchi wanaotumia na kumiliki eneo hilo la Star City, RC Shigela , amesema mgogoro huo umeisha na hataki kuusikia tena katika kichwa chake zaidi ya kutaka kuona maendeleo yanafanyika katika eneo hilo.
RC Shigela, amesema mgogoro huo ulidumu kwa muda mraefu lakini sasa ufumbuzi umepatikana na wananchi wamepatiwa hekari hizo ili waweze kufanya maendeleo.
Hata hivyo, amesema kuwa hatarajii kusikia tena mgogoro huo ukizungumziwa huku akiwataka wananchi wanaoishi katika shamba hilo wawe na subira wakisubiria Manispaa kuaandaa utaratibu mzuri wa kupima viwanja na jinsi ya kuweza kuupanga mji huo.
" Mgogoro tumeumaliza, kilichobakia ni yale maamuzi ambayo tumekubaliana hapa ya Manispaa kuandaa mpango mzuri wa kupima eneo hili na niwaombe sana wananchi tumemaliza mgogoro sitarajii kurudi tena hapa kutatua mgogoro nataka nikija tena nikute huduma za afya zipo, barabara nzuri na mpangilio mzuri wa makazi ili tuweze kusonga mbele katika kuelekea kuwa Jiji" Amesema RC Shigela.
Sambamba na hayo, RC Sanare, ametoa onyo kwa wananchi wanaojimilikisha na kuuza ardhi nje ya taratibu zilizowekwa na Serikali na kuwataka kufuata sheria ili kuepukana na changamoto zinazoweza kujitokeza.
Katika utatuzi wa mgogoro huo, maamuzi yaliyofikiwa ni kwamba katika zoezi la kupima na kugawa ardhi , Manispaa ya Morogoro watanufaika kwa asilimia 45 huku wananchi wakinufaika kwa asilimia 50 na asilimia 5 zitatumika kwa ajili ya huduma za kijamii.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi wa eneo hilo la Kiegea Star City, akiwemo Bw, Anthony Hoza ametoa pongezi kwa Mkuu wa Mkoa huyo kwa kutatua mgogoro huo uliokuwa ukitishia Amani .
Naye, Fatma Athumani amesema mgogoro huo ulikuwa unamkosesha amani kutokana na uvamizi wa ardhi uliokuwepo ambao ulikuwa unapelekea ugomvi baina ya pande hizo mbili kwa maana ya wananchi wa mmiliki wa eneo hilo la Star City.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa