Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), JajiSemistocles Kaijage amesema, uandikishaji wa wapiga kura kwa majaribio katikaKata ya Kihonda, Manispaa ya Morogorounaendelea vyema kutokana na idadi kubwa yawatu wenye sifa waliojitokeza katika vituo kumi vilivyoainishwa.
Jaji Kaijage alisemahayo mara baada ya kukagua zoezi la uandikishaji wa wapiga kura kwamajaribio katika vituo 10 vilivyopo Kata ya Kihonda , Manispaa yaMorogoro.
“ Uandikishaji wa wapiga kura kwamajaribio kata ya Kihonda kwenye vituo vyote10 , mwitikio ni mkubwa na niseme uwakilishi umekuwa mzuri kwa akinamama na vijana wamejitokeza kujiandikisha kwa wingi“ alisema Jaji Kaijage.
“ Watu ni wengi kwakila kituo , hasa kwa vijana wakiume na wakike wao wamejitokeza zaidi “alisema Mwenyekiti wa Tume Jaji Kaijage .
Alisema ,uandikishaji huo unalengakatika kuvifanyia majaribio vifaa vya (BVR) ambavyo vilitumika uchaguzi wamwaka 2015 na mfumo wa uandikishaji wapiga kura ili kubaini changamoto kabla yakuanza kwa zoezi rasmi la uadikishaji wapigakura baadaye mwaka huu.
Uandikishaji wa wapiga kura kwamajaribio ulianza Machi 29 hadi kufikia Aprili 4,mwaka huu, unafanyika katika vituo 20 kwenye kata mbiliya Kihonda , Manispaa ya Morogoro na ya Kibuta ya halmashauri ya wilaya yaKisarawe , mkoani Pwani na kila kata ina jumla ya vituo 10 vyakuandikisha wapiga kura wapya.
Kwa upande wao wananchiwaliojiandikisha siku ya kwanza ya zoezi hilo wanaishi mitaa yaKilombero , Ofisi ya Kata pamoja na Azimio shule ya Msingi kwa nyakati tofautiwaliishukuru Serikali na tume hiyo kwa kuiteua Kata yao kuwa yamajaribio ya uandikishaji na wameweza kupatakipambulisho cha mpiga kura .
Mkazi wa mtaa wa Kilombero ,Sharrifa Thabiti alisema ,hakuwahi kuwa na kitambulisho hicho kabla ya uchaguziwa 2015 na alishindwa kutumia haki yake ya msingi ya kupiga kuralicha ya huduma nyingine za kijamii.
Naye mkazi wa mtaa wa AzimioShuleni , Jema Haruna alisema , anayofuraha kupata kitambulisho cha mpigakura baada ya kushindwa kukipata huko nyuma .
“ Kitambulisho hiki mbali yakutumika wakati wa uchaguzi , pia ni moja ya nyenzo muhimu ya kupata hudumahasa za kifedha , ni vyema wasiokuwa nayo wajitokezakuvipata “ alisema Haruma.
Kwa upande wake Prica Samwel mkaziwa mtaa wa Azimio licha ya kuishukuru Serikali kuwaletea zoezi hilo aliwashauriwatu wanashi katika kata ya Kihonda wajitokeza kutumia muda uliopangwakujiandikisha na kupata vitambulisho hivyo.
“ Vitambulisho vya mpigakura ni muhimu kwa faida yetu sote “ alisema mkazi wa mtaa huo.Katika zoezi hilo watu 12,367wanatarajiwa kuandikishwa kutoka vituo 10 vilivyopo kwenye mitaakumi ya kata ya Kihonda iliyopo Manispaa ya Morogoro.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa