MKUU waWilaya ya Morogoro, Mhe. Bakari Msulwa, amelitaka zoezi la ugawaji wa Vizimbavya Wafanyabiashara katika Soko Kuu la Kisasa Manispaa ya Morogoro lifanyikekwa utulivu na amani.
Kaulihiyo ameitoa jana Julai 23,2020 wakati wa mkutano na Wafanyabiashara wa Soko laManzese katika kuwapa utaratibu ambao Manispaa ya Morogoro umeupanga.
Akizungumzana Waandishi wa habari, Msulwa, amesema kuwa Serikali imewekeza fedha nyingikatika Soko hilo hivyo itakuwa ni jambo la aibu zoezi hilo kama litatawaliwa navurugu na fujo.
Msulwa,amesema kabla ya zoezi la kuwaingiza Wafanyabiashara hao Sokoni lazima waanzekutengenezewa namba zao na kuoneshwa maeneo watakayokaa katika vizimba vyao iliwakati wa zoezi kusiwe na fujo wala viashiria vya uonevu.
"Nimesikiakwamba kuna utaratibu wa wafanyabiashara kuingia hapa Sokoni, lakini niwaombe wahusikahuu utaratibu ili ufanyike vizuri wachukueni wale ambao wameshakuwa katikavigezo vyenu mkawaoneshe Vizimba vyao kwanza kisha muwape namba zao na waleambao watakosa sifa muanze utaratibu wa kuwapa hizo fomu bila upendeleo ili haowenye sifa wakishaingia na hawa wasikose maeneo ya kufanya biashara iliwaendelee kutafuta ridhiki zao, itakuwa jambo la aibu zoezi hili likatawalia navurugu, tutakuwa hatujamtendea haki Mhe. Rais wetu Dkt John Pombe Magufuli kwakutupatia heshima kubwa ya mradi huu ambao ndio mkombozi wa Manispaa yetu"Amesema DC Msulwa.
Katikahatua nyingine, Msulwa, amesema Serikali ipo makini sanana haitofumbia macho chokochoko zenye viashiria vya uvunjifu waamani katika Soko hili.
NayeKaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro ..... amesema wamejipanga vizurikatika zoezi la ugawaji wa Vizimba huku akisema ushauri wa Mkuu wa Wilayawameupokea na kuufanyia kazi kwa ajili ya masilahi ya Serikali naWafanyabiashara watakaokuwa wanafanya biashara katika Soko hilo bila upendeleowowote.
"Tumejipangavizuri sana, utaratibu wa kuwaorodhesha wale wafanyabiashara waliosainimkataba awali kupisha ujenzi wa Soko hili umekamilika mpaka sasa tuna jumla yawafanyabiashara 764 ambao wanatokea Soko la Mawenzi na Manzeseambao tuliwaondoa Soko la zamani kupisha ujenzi wa Soko hili na wale wataokosasifa za kuingia kama ulivyotuelekeza tutaanza haraka zoezi la ugawaji wa fomuna tutalisimamia vizuri kwa umakini bila upendeleo ili nao wawe na sifa zakufanya biashara katika Soko hili"" Amesema Dr Kagize.
Dr Kagize, amewataka Wafanyabiashara hao wa Manispaa ya Morogoro, kuwa watulivu kwani soko hilo linavyovizimba vya kutosha.
Kwaupande wa Mweka hazina wa Manispaa ya Morogoro , Ponceano Kilumbi,amesema mpaka sasa jumla ya wafanyabiashara 764 ndio wamekuwa na sifa zakupata Vizimba Sokoni hapo, ambapo Soko la Manzese ni wafanyabiashara 446wamehakikiwa wenyesifa ni 399 wasio nasifa 47 na Soko la Mawenzi waliohakikiwa398 wenye sifa 365 na wasio na sifa 33.
Kilumbiamesema vizimba vipo 900 wakati idadi ya wafanyabiashara wanaotakiwa kupata Vizimba ndani ya soko hilo ni 764 waliokuwa na wasiona sifa 80 ambapo hesabu inayoonyesha kuwa vizimba 136 vitabaki bila kutumika.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa