MKUU WA WILAYA YA MOROGORO MHE. REBECA NSEMWA, ANAWATANGAZIA WANANCHI WOTE WA MANISPAA YA MOROGORO KUWA KESHO MEI 13/2023 , MANISPAA YA MOROGORO ITAPOKEA MWENGE WA UHURU KITAIFA KATIKA UWANJA WA MPIRA WA MIGUU SHULE YA SEKONDARI MAFIGA.
MUDA WA MAPOKEZI NI SAA 12:00 ASUBUHI.
MIONGONI MWA MAENEO AMBAYO YATAPITIWA NA MWENGE WA UHURU KITAIFA 2023 NI SOKO LA MAWENZI( KUFANYA USAFI NA WANANCHI WA ENEO HILO LA SOKO
), UPANDAJI MITI 2000 ENEO LA BWAWA LA MINDU, UZINDUZI WA MRADI WA UBORESHAJI HUDUMA YA MAJI KAUZENI, KUONA SHUGHULI ZA KIKUNDI CHA WAJASILIAMALI CHA UOTESHAJI MICHE MADIZINI KATA YA BOMA, KUWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA KITUO CHA AFYA TUNGI, KUONA SHUGHULI ZA KIKUNDI CHA VIJANA CHA OKOA GROUP CHA KUTENGENEZA CHAKI NANENANE KATA YA TUNGI, KUONA KIWANDA CHA KUCHAKATA TAKA ZA PLASTIC KATA KIHONDA MAGHOROFANI, KUWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA JENGO LA UTAWALA SHULE YA SEKONDARI MKUNDI MLIMANI.
KATIKA ENEO LA MKESHA TUMBAKU SHUGHULI ZIFUATAZO ZITAFANYIKA IKIWA NI
PIA KATIKA MKESHA HUO, KUTAKUWA NA BURUDANI MBALIMBALI IKIWEMO MZIKI WA SINGELI, LIVE BAND, VIKUNDI VYA NGOMAA NA WASANII MBALIMBALI WA KUBURUDISHA.
WANANCHI WOTE MNAKARIBISHWA NA KUJITOKEZA KWA WINGI KWA KILA ENEO AMBALO MWENGE UTAPITA.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa