MANISPAA ya Morogoro imeendesha mafunzo ya maboresho katika Mfumo wa Uhasibu na Utoaji wa Taarifa za kifedha katika Vituo vya kutolea huduma (Effars).
Mafunzo hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Mbaraka Mwishehe DDC Agosti 18-2025 ambapo yatafanyika kwa siku mbili mpaka Agosti 19-2025.
Akizungumza katika mafunzo hayo, Mhasibu wa Manispaa ya Morogoro,Mussa Mshana, amesema mafunzo hayo yemelenga zaidi kwa Waalimu wa fedha wa Shule za Msingi, Sekondari na Vituo vyote vya kutolea huduma za afya.
Mshana ,amesema vituo vya kutolea huduma, kama vile zahanati, vituo vya afya na shule za msingi na sekondari, ni taasisi za umma zilizo na jukumu la kutoa huduma ya moja kwa moja kwa wananchi katika maeneo yao.
Aidha, Mshana ,amesema , fedha za kugharamia utoaji wa huduma katika jamii zinatokana na vyanzo mbalimbali, vikijumuisha tozo au michango ya bima za afya kutoka kwa watumia huduma, na ruzuku ya Serikali na Washirika wa Maendeleo.
Hata hivyo,amesema mfumo huo wa FFARS umetayarishwa ili kukidhi mahitaji ya stadi sahihi (zilizoboreshwa) za udhibiti wa fedha katika ngazi ya kituo
“vituo vimekuwa na changamoto ambayo imekuwepo kwa muda mrefu kama vile uwepo wa mifumo mbalimbali ya kisekta ya uhasibu/udhibiti wa fedha, kukosekana kwa utaratibu mzuri na jumuishi wa utoaji wa taarifa za fedha jambo ambalo linapelekea taarifa za fedha za halmashauri ambazo sio kamili na ndio maana wameona umuhimu wa kutoa mafunzo hayo.
Faida za mafunzo hayo ni malipo kufanyika kwa haraka zaidi ukiliganisha na sasa, ulinzi na usalama wa taarifa za malipo ya wateja,uzingatiaji wa sera,, sheria , kanuni na usimamizi wa matumizi ya fedha za Serikali.
Mafunzo hayo yataendelea Agosti 19-2025 yakijumuisha waalimu wa fedha Shule za Sekondari pamoja na watoa huduma wa vituo vya afya.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa