UTARATIBU WA KUPATA LESENI ZA BIASHARA.
Leseni za biashara hutolewa na wakala wa usajili wa biashara na leseni (Brela). Halmashauri za Manispaa, majiji, miji na zawilaya kwa kuzingatia kundi la leseni inayotolewa.
Leseni za biashara zimegawanyika katika makundi mawili A na B.
KUNDI A
kuna biashara ambazo leseni zake hutolewa na wakala wa biashara na leseni (Brela).kundi hili ni leseni zenye mtaji mkubwa zinazojumuisha leseni za uuzaji wa bidhaa za nje ya nchi, huduma za mawasiliano, bandari, vilabu vya usiku, sonara, uchimbaji madini, uuzaji na usambazaji silaha, vyombo vya habari, hoteli za kitalii, huduma za kifedha, taasisi za kifedha na mitaji,bima n.k
KUNDI B
Leseni zinazotolewa na Halmashauri za Manispaa, majiji, miji na zawilaya.
Katika kundi B kuna biashara za viwanda vidogo, hoteli zisizo za kitalii, vyama vya ushirika, makumpuni ya ujenzi, taaluma muhimu, zahanati, maduka ya dawa muhimu za binadamu, pembejeo za kilimo, migahawa,kalakana, uandishi wa vitabu na magazeti, vituo vya mafuta, spea mbalimbali, shule za binafsi, minada, pembejeo za kilimo, wahandisi wa umeme, maduka ya kuuza bidhaa kwa jumla na rejareja n.k
Biashara za kundi B leseni zake hutolewa na Halmashauri ya eneo husika ambapo biashara inafanyika
JINSI YA KUOMBA LESENI YA BIASHARA
Mfanyabiashara anatakiwa kujaza fomu ya maombi ya biashara ambayo hupatikana katika Halmashauri husika
Nyaraka muhimu zinazotakiwa,
Baada ya kukamilisha nyaraka zote mteja atapewa bili (invoice)kulingana na aina ya biashara yake na kwenda kulipia benki
Mchakato hukamilishwa kwa mteja kuchukua leseni yake na kupewa maelezo/ elimu ya uendeshaji biashara.
KUMBUKA
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa