• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Morogoro Municipal Council
Morogoro Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
    • Wakuu wa Divisheni na Watumishi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Divisheni
      • Rasilimaliwatu na Utawala
      • Miundombinu, Uendelezaji wa Vijijini na Mijini
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe
      • Mipango na Uratibu
    • Vitengo
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Ugavi na Manunuzi
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Fedha na Uhasibu
      • Taka Ngumu na Usafishaji
      • Michezo, Sanaa na Utamaduni
      • TEHAMA
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Viwanda
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Mazingira
    • Miundombinu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao Vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Meya/Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Iliyoisha
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Fomu ya Maombi
    • Waraka
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Picha
  • Market
    • Market line 1
    • Maket line 2

DC KILAKALA AWATAKA WANANCHI KUFICHUA WAHARIFU WA VITENDO VYA UKATILI DHIDI YA WATOTO

Posted on: June 17th, 2025

MKUU wa Wilaya ya Morogoro Mhe.Mussa Kilakala,amewataka wananchi kuwafichua wanaotenda makosa ya ukatili dhidi ya Watoto katika Jamii.

Kauli hiyo ameitoa Juni 16-2025 katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika Manispaa ya Morogoro iliyofanyika eneo la Uwanja wa Mpira wa Miguu Shule ya Msingi Mwembesongo.

Akizungumza na wananchi waliojitokeza katika maadhimisho hayo,DC Kilakala,amesema siku ya Mtoto wa Afrika ni vyema jamii ikafanya tathimini ya hali halisi iliyopo kwa kutafakari Kauli mbiu ya Siku ya Mtoto wa Afrika mwaka 2025 inayokumbusha kuangalia mienendo dkatika makuzi na malezi ya Watoto wakiwa nyumbani, nje ya nyumbani kwa kuangalia walipotoka,walipo na wanapoenda na kurekebisha mapungufu ili kuangalia kesho yao kwa malezi bora.

Aidha ameiomba Jamii kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kuhakikisha vitendo vya ukatili dhidi ya Watoto vinakemewa vikali na kuzuiwa katika Jamii.

DC Kilakala, amewataka wazazi/walezi na wadau wa masuala ya Watoto kwa kila mmoja aone kwamba ana wajibu wa kuleta mabadiliko chanya kwa jamii kushiriki kikamilifu katika kulinda na kutekeleza kwa vitendo Haki za Watoto.

“Tuna wajibu wa kutoa elimu kwa Watoto wetu juu ya mabadiliko mbalimbali ya kijamii ikiwemo matumizi ya teknolojia ambapo ukuaji wake uendane na ukuaji wa elimu ili matumizi yake yasiwe na athari hasi katika maendeleo ya ukuaji na hatma ya Maisha ya watoto wetu” Amesema DC Kilakala.

Mwisho,ameitaka Jamii kukabiliana na mmomonyoko wa maadili kwa kukemea hali ya ukiukwaji wa maadili mema hususani katika kuingiza mila,desturi na tamaduni zisizokubalika na kulinda mila na desturi nzuri kwa Watoto na jamii kwa ujumla.

Naye Mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Morogoro,Faraja Maduhu,amesema siku hii huadhimishwa kwa lengo la kutambua thamani,utu na umuhimu wa Mtoto Duniani kutokana na mauaji ya Watoto takribani 2000 yaliyofanywa na utawala wa Makaburu katika Kitongoji cha Soweto Nchini Afrika Kusini tarehe 16,Juni mwaka 1976.

Maduhu amesema Kauli Mbiu ya mwaka 2025 inaitaka Jamii kutafakari upatikanaji wa haki haki za Watoto tangu zilipoanzishwa na Sera ya Maendeleo ya Mtoto yam waka 2008 ambayo inakumbusha wazazi au walezi na jamii haki tano za msingi za mtoto ikiwemo kuishi, kulindwa, kuendelezwa,kutobaguliwa na haki ya kushiriki na kutoa maoni kwa mambo yanayomuhusu.

Kwa upande wa Mratibu wa Dawati la Maendeleo ya Mtoto Manispaa ya Morogoro,Joyce Mugambi,amesema elimu za kupinga ukatili ulitolewa kwa Kata 12 na kufikia shule za Msingi 14 na vituo vya kulelea Watoto 4 ,kutoa elimu Kamati za usalama shuleni kwa Zaidi ya shule za Msingi 128,kuhuisha Mabaraza ya Kata 23 na Mitaa 135 ,kutoa elimu juu ya haki na wajibu ambapo jumla ya shule 17 za Msingi na wanafunzi Zaidi ya 658 wamefikiwa na elimu hiyo.

Kauli Mbiu ya Siku ya Mtoto wa Afrika mwaka 2025 inasema “Haki za Mtoto:Tulipotoka,Tulipo na Tuendako”.


Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 04, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI February 19, 2025
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2023 July 14, 2023
  • ENVIRONMENT AND SOCIAL IMPACT ASSESSMENT April 24, 2024
  • Angalia Yote

Habari Mpya

  • WIZARA YA MAJI YADHAMIRIA KUTATUA CHANGAMOTO YA MAJI MOROGORO-ENG.MWAJABU.

    July 03, 2025
  • . RAS MOROGORO AFUNGA MAFUNZO YA PEPMIS, ATAKA UWAJIBIKAJI NA UAMINIFU

    June 30, 2025
  • KAMATI YA CHAKULA NA VIPODOZI YATAKIWA KUJIKITA KATIKA UTOAJI WA ELIMU KWA WAFANYABIASHARA.

    June 20, 2025
  • DC KILAKALA AWATAKA WANANCHI KUFICHUA WAHARIFU WA VITENDO VYA UKATILI DHIDI YA WATOTO

    June 17, 2025
  • Angalia Yote

Video

MEYA KIHANGA AKABIDHI TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI ZAIDI YA 1600 WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Leseni za Biashara
  • Sheria Ndogo za Manispaa ya Morogoro
  • Sisi ni Nani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Tamisemi
  • Morogoro Modern Market system (outside)
  • Tovuti ya Utumishi
  • Morogoro Modern Market System (LAN Network)
  • Tovuti Rasmi ya Ikulu
  • Tovuti ya RAS Morogoro

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro

    Anuani: 166 morogoro

    Simu: 0232614727

    Simu: 0734-039300

    Baruapepe : info@morogoromc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa