KATIBU Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Alhaji Dkt. Mussa Ali Mussa,amewataka watumishi wa umma mkoani humo kuwajibika na kuwa waaminifu katikakujaza mfumo wa mwongozo wa utekelezaji wa usimamizi wa utendaji kazi (PEPMIS),ili kuhakikisha mkoa huo unatekeleza kikamilifu agizo la Serikali.
Dkt. Mussa alitoa kauli hiyo tarehe 28 Juni 2025, wakatiakifunga mafunzo ya siku sita kuhusu ujazaji wa mfumo huo wa PEPMIS,yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro,ikiwa ni siku ya mwisho ya mafunzo hayo mkoani humo.
Amesema kuwa wakuu wa seksheni, idara na vitengo wasipokuwawaaminifu na kuruhusu ujazaji holela wa taarifa katika mfumo huo, itakuwavigumu kufikia malengo ya Serikali.
Aliongeza kuwa viongozi hao watakuwa wameshiriki moja kwa mojakatika kuushusha mkoa huo kiutendaji, ambao kwa sasa uko nafasi ya pili kitaifakwa ujazaji wa mfumo wa PEPMIS, na kwa upande wa vyuo, Mkoa wa Morogoro ndiokinara.
“Ombi langu sasa, kila mmoja atimize wajibu wake anavyotakiwa…tujaze fomu hizo kwa mantiki kwamba kila mmoja anajaziwa kwa kileanachostahili,” alisisitiza Dkt. Mussa.
Mafunzo hayo ya PEPMIS yalianza tarehe 23 Juni 2025, yakitolewana maofisa kutoka Ofisi ya Rais – Utumishi, yakiwahusisha makundi mbalimbali yawatumishi wa umma, hususan wakuu wa idara na vitengo kutoka halmashauri za mkoahuo, Sekretarieti ya Mkoa, na taasisi za umma zilizoko mkoani humo.
Mfumo wa utendaji kazi, yaani Performance ManagementInformation System (PEPMIS), una lengo la kuongeza ufanisi na uwajibikajikwa watumishi wa umma.
Pia ni mfumo huo nyenzo muhimu ya kiutumishi inayosaidiamtumishi wa umma kuweka malengo yake ya utendaji kazi na kuyatekeleza ipasavyo.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa