Baraza la Madiwani Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro limepitisha bajeti ya shilingi 93,809,858,854.97 kwaajili ya kutekeleza shughuli za maendeleo na matumizi ya kawaida kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
Bajeti hiyo imeridhiwa katika kikao maalum cha Bajeti cha Baraza la Madiwani kilichofanyika tarehe Februari 18,2025 katika ukumbi wa Mikutano wa Manispaa.
Akiwasilisha mapendekezo ya mpango wa Bajeti ya mwaka wa fedha 2025/2026 kwa niaba ya Mkurugenzi Ndg.Edward Mwamotela ambae ni mkuu wa divisheni ya Mipango ameeleza kuwa bajeti hii imejikita katika kuongeza mapato ya ndani,kuboresha miundombini ya kutolea huduma za Afya na Elimu,kuboresha miundombinu ya barabara,uwezeshaji wananchi kiuchumi,utawala bora,usafi wa mji,utunzaji wa Mazingira na kuboresha miundombinu ya kiuchumi.
Aidha ameeleza Manispaa ya Morogoro inatarajia kukusanya na kutumia kiasi shilingi Bilioni 93,809,858,854.97 ambapo kiasi cha Bilioni 15,622,877,000.00 ni Mapato ya vyanzo vya ndani vya Halmashauri,shilingi 65,817,912.000.00 ni Mishahara,shilingi 2,346,829,000.00 ni Matumizi mengineyo,shilingi 6,431,989,256.00 ni Ruzuku ya Miradi ya maendeleo, na shilingi 4,377,166.000 ni wadau wa maendeleo.
Kwa upande wa Diwani wa Kata ya Uwanja wa Taifa Mhe. Rashid Matesa amewapongeza watendaji wa maandalizi mazuri ya Bajeti ambayo imegusa kila sekta kuanzia elimu,afya na miundombinu na kuwataka Watendaji kuwajibika ipasavyo ili kuboresha utendaji kazi na kwa maslahi ya umma.
Aidha Diwani wa Kata ya Mji Mpya Mhe.Emmy Kiula ameipongeza Menejimenti kwa kutenga fedha za kufanya ukarabati wa soko la Mawenzi na Kuomba bajeti ijayo soko la Mjimpya liweze kuingizwa katika bajeti ili kufanyiwa ukarabati.
Naye Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Morogoro,Mhe,Fikiri Juma amewapongeza wataalam kwa maandalizi mazuri ya Bajeti na kuelekeza kuwa Manispaa ya Morogoro inaelekea kuwa Jiji hivyo katika vipaumbele vyake ni vyema tukazingatia uwekaji wa Bustani katika maeneo ya wazi.
Pia Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro Ndg.Emmanuel Mkongo amewaahidi waheshimiwa Madiwani kuyafanyia kazi yale yote yaliyoagizwa na Baraza la Madiwani.
Katika kuhitimisha mkutano huo Mstahiki Meya amewataka watendaji kuhakikisha bajeti iliyopitishwa ikatumike kama ilivyopangwa ili kuwaletea maendeleo wananchi wa Manispaa ya Morogoro.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa