MANISPAA ya Morogoro imeadhimishaWiki ya Unyonyeshaji wa Maziwa ya Mama Duniani yanye lengo la kutoa hamasa kwa jamii katika kulinda, kuimarisha nakuendeleza unyonyeshaji wa watoto.
Maadhimisho hayo yamehitimishwa na Mkuu waWilaya ya Morogoro,Mhe.Mussa Kilakala,Agosti 07-2025 katika Ukumbi wa KilakalaSoko Kuu la Chifu Kingalu Morogoro.
Akizungumza juu ya maadhimisho hayo, DCKilakala, amewataka wakina mama wote ambao wamejifungua watoto na wanaotarajiakujifungua kutoa kipaumbele katika suala la unyonyeshaji wa ziwa la mama kwanifaida zake huchangia katika uchumi wa nchi.
Aidha, DC Kilakala,ametoa wito kwa watoa hudumawa afya na wahudumu wa afya ngazi ya jamii kuendelea kuhakikisha wanafikiajamii na elimu ya unyonyeshaji wa ziwa la mama ,lishe na afya kwa ujumlainatolewa ipasavyo.
DC Kilakala,amempongeza Mkurugenzi wa Manispaaya Morogoro kwa kutambua umuhimu katika kuhudumia jamii na kuhakikisha katikakilele cha maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji anawajengea uwezo zaidikuhusiana na ulishaji wa watoto wachanga na wadogo ambapo unyonyeshaji wa ziwala mama ni mada muhimu ndani yake.
Naye Mkuu wa Divisheni ya Afya,Ustawi wa Jamiina Lishe Manispaa ya Morogoro, Dkt.Maneno Focus, amewataka watoa hudumawahakikishe maeneo waliyopo wanawawezesha jamii kutambua umuhimu wa ziwa lamama na kuhakikisha ufanishaji wa ziwa la mama unazingatiwa.
Mratibu wa Kitengo cha Lishe Manispaa yaMorogoro, Ester Kavishe,amesema mtoto akizaliwa ndani ya lisaa limoja anyonyeshweapate maziwa ya awali ya majimaji ya njano yanayoitwa kolostaramu ambayo nibora sana kwa mtoto ambao katika kipindi cha miezi sita anyonyeshwe ziwa lamama pekee bila kupewa chakula chochote.
Kavishe,amesema maziwa ya mama ni chakula borakwa mtoto kwani humpa mtoto virutubisho vyote kwa uwiano sahihi na pia majikatika miezi sita ya mwanzo.
Mwakilishi wa wazazi,Anna Mwakipesile,amesematangia ajifungue amekuwa akizingatia mlo kamili na unyonyeshaji sahihi kitukilichofanya watoto wake kuwa na afya njema kutokana na kuzingatia makundi sitaya chakula.
Maadhimisho ya Wiki ya Unyonyeshaji wa Maziwaya Mama Duniani, yamebeba Kauli Mbiu ya wiki ya unyonyeshaji mwaka 2025"Thamini Unyonyeshaji: Weka mazingira wezeshi kwa mama na mtoto"ambapo Maadhimisho hayo yyalianza tarehe 1 - 7 Agosti, 2025 kupitiavituo vyote vya kutolea huduma za Afya.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa