MSIMAMIZI wa Uchaguzi Jimbo la Morogoro Mjini, Elizabeth Ngobei, amewataka wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Kata kusimamia kanuni na sheria za uchaguzi ili kuepuka na migogoro isiyo ya kilazima katika maeneo yao ya kupigia kura.
Ameyasema hayo katika kuhitimisha rasmi kwa mafunzo ya wasimamizi wa Uchaguzi ngazi ya Kata yaliyoanza tarehe 4 hadi tarehe 6 Agosti katika ukumbi wa Mbaraka Mwishehe DDC Manispaa ya Morogoro.
“Mmemaliza mafunzo haya ,rai yangu nendeni mkahakishe mnasoma miongozo na kanuni za Uchaguzi ipasavyo na kuelewa ili waweze kutekeleza majukumu yao pasi na shaka lakini mshirikishe vyama vya siasa kwa kila hatua pamoja na kushirikisha wadau wa uchaguzi kwa ukaribu pamoja na kuwapa ushirkiano waangalizi wa uchaguzi”Amesema Ngobei.
Aidha, Ngobei, amewapongeza wakufunzi na washirki wote wamafunzo na kuwataka kutekeleza wajibu wao kwa kutoa mafunzo kwa vitendo kwa wasimamizi wa vituo, wasimamizi wasaidizizi na makarani wahamasishaji wa wapiga kura.
Pia,amewataka wasimamizi hao kuhakikisha wanabandika orodha yote ya wapiga kura kwenye ubao wa matangazo pamoja na kutoa fomu za uteuzi za Madiwani na uteuzi wa Madiwani ufanyike kwa mujibu wa sheria.
Mwisho,amesisitiza suala zima la kutunza siri katika shughuli nzima ya Uchaguzi ili kuweza kuzuia taharuki ambazo zitazorotesha amani na utulivu katika zoezi hilo la Uchaguzi.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa