Kamati ya Mipangomiji na Mazingira Manispaa ya Morogoro imeridhishwa na utekelezaji wa miradi ya Uboreshaji Miji (TACTIC) inayotekelezwa na Manispaa ya Morogoro.
Kamati hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti wake, ambaye ni Diwani wa Kata ya Mwembesongo, Mhe. Ally Kalungwana, Julai 24-2024 imefanya ziara na kukagua baadhi ya miradi ya TACTIC ikiwemo ujenzi wa barabara za Tungi, Kihonda na Mazimbu, na eneo linalotarajiwa kujengwa Stendi ya kisasa eneo la Stesheni ya SGR.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Kalungwana , amesema kamati hiyo imeridhishwa na utekelezaji wa miradi waliyoitembelea, na kuutaka uongozi wa Manispaa ya Morogoro kuendelea kusimamia miundombinu hiyo isiharibike ili kutoa huduma bora kwa wananchi.
Manispaa ya Morogoro ni moja ya Halmashauri ambayo inatekeleza miradi ya TACTIC ikiwa na lengo la kuboresha miundombinu ya miji na kuimarisha utoaji wa huduma kwa jamii.
Manispaa ya Morogoro imepokea Bilioni 19, 606,559.46 kutoka Serikali Kuu kutekeleza miradi ya TACTIC.
Miongoni mwa miradi ya TACTIC ni Ujenzi wa Barabara ya Muhimbili, Tubuyu II, Mjimwema, Barakuda, Kihonda-VETA na Ujenzi wa mifereji ya maji (ANT Mlaria na Kikundi).
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa