Katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya Wanawake duniani ambayo uhadhimishwa Duniani kote kila ifikapo Machi 8,Wilaya ya Morogoro imeadhimisha siku ya Wanawake kwa kufanya matendo ya huruma kwa wahitaji mbalimbali katika jamii,kutoa elimu ya usawa wa kijinsia,mbio za pole na maonyesho ya bidhaa mbalimbali za majukwaa ya wanawake.
Maadhimisho hayo yamefanyika Machi 4/2025 katika ukumbi wa Chilakale yakiambatana na Maandamano.
Akizungumza katika maadhimisho hayo Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mhe.Musa Kilakala amewapongeza wanawake wote waliojitokeza kuadhimisha siku ya wanawake Duniani na kueleza kama kauli mbiu isemavyo “WANAWAKE NA WASICHANA 2025;TUIMARISHE HAKI USAWA NA UWEZESHAJI” hivyo amewasisitiza kuhusu kuelimisha ,kuhimiza umma juu ya umuhimu wa utekelezaji wa Ajenda ya usawa wa kijinsia haki na uwezeshaji wa wanawake na wasichana katika maendeleo ya kijamii,kiuchumi na kisiasa.
“Nawapongeza kwa kutekeleza kwa vitendo kauli mbiu hii ya mwaka huu kwa kuungana Pamoja wanawake ,wanaume na Watoto katika shughuli za kijamii hii inaonesha mshikamano mkubwa uliopo,pia nichukue fursa hii kuwakumbusha kuendelea kukemea kwa nguvu zote vitendo vya ukatili wa kijinsia vinavyoendelea katika jamii yetu”Amesema DC Kilakala.
Aidha DC Kilakala amewakumbusha wanawake kuwa Serikali imetoa maelekezo ya utoaji wa mikopo ya asilimia 10 na kundi la wanawake upata asilimia 4,hivyo amewataka wanawake wanapopewa mikopo hiyo kuitumia kwa lengo lililokusudiwa na kuwa waaminifu na kurejesha fedha walizokopeshwa kwa wakati.
Pia Dc Kilakala ametoa wito kwa wanawake wao kama nguzo za familia kuhakikisha wanajiunga na Bima ya Afya iliyoboreshwa(ICHF) ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za matibabu pindi yanapohitajika.
Naye Mkaguzi msaidizi Kata ya Lukobe Bi Zuwena Mwita,amewaasa wanawake kutoa taarifa ya matendo ya ukatili wa kijinsia ili sheria iweze kuchukua mkondo wake,na ameeleza kwa sasa ukatili wa kijinsia umegeuka ata wakina baba wanatendewa matendo ya ukatili hivyo ameiasa jamii kutofumbia macho matendo maovu.
Maadhimisho haya ya siku ya Wanawake Duniani kimkoa yatafanyika Wilaya Ifakara Machi 8,2025.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa