HALMASHAURI ya Manispaa ya Morogoro imefanya maboresho makubwa katika mfumo wa kujiendesha kisasa wa kutumia Vishikwambi kwa lengo la uwasilishaji wake wa taarifa hususani katika Vikao vya Mabaraza ya Madiwani.
Uzinduzi huo wa mafunzo ya Vishikwambi umefanyika Desemba 16/2022 katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi Kuu ya Manispaa.
Akizungumza katika uzinduzi wa mfumo wa kijigitali mara baada ya kugawa Vishikwambi kwa Madiwani na Wakuu wa Divisheni na Vitengo , Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Hilary Sagara, amesema matumizi ya Vishikwambi yanalenga kuongeza ufanisi wa kazi na kuokoa fedha ambazo zimekuwa zikitumiwa kuchapisha makabrasha.
Sagara, amesema faida nyengine ya Manispaa kujiendesha Kijigitali ni kusaidia kuokoa muda wa kuandaa makabrasha ya Madiwani wakati wa vikao.
" Nichukue nafasi hii kuwapongeza Manispaa ya Morogoro kwa kuja na mpango bora wa mapinduzi ya kijidigitali, dunia sasa ipo Kijidigitali, vishikwambi hivi vitasiaida kuokoa fedha za machapisho ya makabrasha ambapo fedha hizo zinaweza kuelekezwa katika matumizi mengine ya maendeleo " Amesema Sagara.
Kwa upande wa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, Mhe. Pascal Kihanga, amewataka Madiwani kuwa waangalifu na vifaa hivyo na kuvitumia kwa matumizi yaliyokusudiwa ili viendelee kuwasaidia.
Naye , Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Ally Machela, amesema uwepo wa vishikwambi utarahisisha taarifa kufika kwa wakati kwa walengwa.
Katika hatua nyengine, Diwani wa Viti Maalum , Grace Mkumbae, amempongeza Mstahiki Meya kwa kuja na wazo hilo pamoja na wataalamu kwa kufanikisha mapango wa Manispaa kujiendesha kisasa.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa