MANISPAA ya Morogoro imefanya kikao cha Kamati ya Ushauri ya Wilaya (DCC) kwenye ukumbi wa Ofisi Kuu ya Manispaa Januari 6/2025.
Lengo la kikao hicho ilikua ni kujadili taarifa mbalimbali zautendaji kazi wa halmashauri na taasisi zote zilizopo ndani ya wilaya ya Morogoro.
Katika Kikao hicho,taarifa ya utekelezaji wa Bajeti iliwasilishwa na Idara ya Mipango na Uratibu na Bw. Edward Mwamotela Afisa Uchumi, inayoonesha malengo na mafanikio ya Mwaka wa Fedha 2023/2024 na bajeti ya mwaka 2024/2025.
Akizungumza katika kikao hicho, DC Kilakala,amewataka wajumbe wa DCC wote kwa kushirikiana na wananchi kuhimizana umuhimu wa kulipa kodi ili miradi ya maendeleo iweze kuimarishwa na kuongeza mapato ya Halmashauri.
Aidha,DC Kilakala,amesisitizia suala zima la kupanga Mji,amesema upo mpango tayari ameshatuma timu ya wataalamu kuangalia eneo la mlapaklolo ili liwe eneo la kupatakana vyakula vyote vinavyopatikana usiku vipatikane sehemu moja ili kufungua mji na kutofanya biashara kila maeneo.
Aidha, DC Kilakala amesisitiza ushirikiano na mahusiano mazuri baina ya Taasisi na Taasisi, kukaa kwa pamoja kujadiliana changamoto mbalimbali zinazojitokeza na kuzimaliza na sio kusubiri Kikao Cha DCC.
Akichangia hoja mmoja wa wajumbe wa kikao hicho Ndg Ismail Ismail Kutoka Chama Cha CHAUMA , ameipongeza Halmashauri kwa ujenzi wa miradi ya maendeleo huku akiomba Uongozi uangalie kwa mapana suala la kodi kwa wafanyabiashara wa Soko la kisasa la Chifu Kingalu.
Naye Ndg. Elizeus Rwegasira Katibu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ameshauri Manispaa badala ya kuwahamisha wafanyabiashara njiani wajue kwanini wanauza hapo na nini kinawapelekea wauze maeneo hayo ikiwemo kuwawekea miundombinu rafiki kwa wateja na wauzaji ili wafanyabiashara hao wafanye biashara zao na kujipatia kipato.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa