Wasimamizi wasaidizi ngazi ya kata Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro wamepewa mafunzo juu ya uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura linalotarajiwa kuanza Machi 1-7,2025.Mafunzo hayo yamefanyika katika katika Ukumbi wa Bwalo la Umwema.
Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo Afisa mwandikishaji ngazi ya Jimbo Ndg.Faraja Maduhu, ameanza kwa kuwapongeza kwa kuteuliwa kuwa waandikishaji wasaidizi na kuwaeleza anatarajia baada ya mafunzo hayo kila alietueliwa atafanikisha kwa weledi zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura.
Aidha ameeleza kuwa mafunzo hayo yanajumuisha utumiaji wa mashine za BVR,na kuwasihi kwa wale ambao waliwah kushiriki zoezi hili katika kipindi kilichopita kuendelea kuwaelekeza waaandikishaji wasaidizi ambao ndio mara yao ya kwanza kushiriki zoezi hili.
Pia alieleza katika uboreshaji huu mawakala wa vyama vya Siasa wataruhusiwa kushiriki kwaajili ya kuwatambua wakazi wa maeneo husika,ila hawataruhusiwa kuingilia shughuli ya uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura.
Naye Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi,Jaji wa Mahakama ya Rufani Mhe.Jacob Mwambengele amewataka washiriki wa mafunzo hayo kuzingatia yale yote wanayofundishwa,kwa kuwa wasikivu na kufuata sheria,kanuni za Uchaguzi.
Aidha amewalekeza wasimamizi wasaidizi ngazi ya kata kuwasiliana na watumishi wa tume huru ya Uchaguzi endapo watakutana na changamoto yoyote wakati wa utekelezaji wa uboreshaji wa daftari la kudumu la Mpiga kura.
Zoezi hili la Uboreshaji wa Daftari la kudumu Mkoa wa Morogoro linatarajiwa kufanyika kuanzia Machi 1-7.2025 na sifa za wanahoitajika kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura ni ambao wametimiza umri wa miaka 18 na kuendelea ambao hawakuandikishwa hapo awali,watakaotimiza miaka 18 kabla ya tarehe ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025,waliojiandikisha awali na wamehama Kata au Jimbo moja kwenda jingine,waliopoteza sifa mfano wale waliofariki kuondolewa katika Daftari,wenye taarifa zilizokosewa wakati wa uandikishaji na waliopoteza au kadi zao kuharibika.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa