MKURUGENZI WA MANISPAA MOROGORO AWATAKA WANANCHI KURASIMISHA MAKAZI YAO.
Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro imewataka wakazi wa mkoa huu,wanaoishi katika maeneo yasiyo rasmi kurasimisha makazi yao ili kuweza kufikiwa na huduma za kijamii.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro Ndg John K.Mgalula wakati akijibu maswali ya papo kwa papo katika kikao cha Baraza la Madiwani lililofanyika tarehe 27/04/2017.
Aidha amesema wanaojenga maeneo yasiyo rasmi ambayo hayajapimwa wana uwezo wa kifedha hivyo ni vyema warasimishe makazi yao ili kuepuka migogoro inayoweza kuepukika.
Hata hivyo amesema kuwa umefika wakati wa Baraza la Madiwani kukubaliana na kuungana na Halmashauri kukataa makazi yanayojengwa katika maeneo ambayo hayajapimwa ili kufikia malengo ya Manispaa kuwa jiji.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa