Mwenge wa Uhuru umepita Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro na kufungua miradi 3,mradi 1 umewekewa jiwe la msingi na miradi 2 imezinduliwa.
Akieleza mbele ya kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Bw Amour Amed Amour,Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Bi Regina Chonjo amesema katika utekelezaji wa miradi hiyo wananchi wamechangia jumla ya Tsh 3,149,665.00,Halmashauri ya Manispaa Tsh 36,000,000.00,Serikali kuu Tsh 821,998,000,00 na wahisani Tsh 12,065,888,000.00
Aidha Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro alitoa ufafanuzi kuwa miradi yote iliyopitiwa na Mwenge wa Uhuru ni katika utekelezaji wa dira ya Maendeleo 2025,ambapo Halmashauri imeweka mikakati ya kutokomeza kabisa umaskini ,maradhi na ujinga miongoni mwa wananchi wake kwa kujiwekea mipango ya utekelezaji wa malengo ya Milenia 2010 MKUKUTA,MKURABITA na ilani ya Uchaguzi ya Mwaka 2015.
Ujumbe wa Mwenge wa mwaka 2017 ni Shiriki kukuza Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo ya nchi yetu.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa