SHIRIKA lisilo la Kiserikali la Mother Of Mercy linatarajia kuzindua mashindano ya Kombe la Nishati safi Manispaa ya Morogoro.
Hayo yamezungumzwa na Mkurugenzi wa Shirika hilo, Ndg. Gration Mbelwa, katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Uwanja wa mpira wa Miguu wa Jamhuri Morogoro Julai 11-2025.
Mbelwa, amesema mshindano hayo yanalenga kuhamasisha wananchi kutumia nishati safi ya kupikia na kuondokana na matumizi ya nishati ya kuni.
Hata hivyo amesema kuwa mashindano hayo yatashirikisha timu 32 ambapo kila Kata itatoa timu moja na timu 3 zitashiriki kwa mfumo wa kualikwa katika mashindano hayo.
"Mashindano yetu tumeshirikisha sana Maafisa watendaji wa Kata ambao wametupatia timu 29, na timu 3 tumezialika, lakini kwa kila timu shiriki tutawapatia jezi na mpira na miche ya miti 500 ili kuipada katika maeneo yao kwa kishirikiana na Maafisa Mazingira, matumaini yetu tutawafikia watu wengi, lengo kumsapoti Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuja na mpango wa matumizi ya nishati safi" Amesema Mbelwa.
Mashindano hayo yanatarajia kuzinduliwa Julai 12-2025 katika Uwanja wa Mpira wa Miguu wa Jamhuri kwa kufanya maandamano ya amani ya madereva wa boadaboda ya kuzunguka mji wa Morogoro kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia ambapo viongozi mbalimbali wa Serikali na Chama.
Licha ya mashindano ya Mpira wa miguu ,Mbelwa, amesema pia kutakuwa na mashindano ya Bodaboda , ambapo mshindi wa mashindano hayo atazwadiwa pikipiki mpya
"Mashindano haya ya bodaboda tutayaendesha kwa mfumo wa kila mwenesha bodaboda atapanda mti mmoja katika mlima wa uluguru na baada ya hapo yule aliyeshinda kwa kutumia muda mfupi katika mbio hizo atakuwa mshindi na atazawadiwa bodaboda mpya na mshindi wa pili atapewa shilingi milioni 1 na mshindi wa tatu atapewa shilingi laki 5 na jumla ya miti watakayopanda itategemea na idadi ya washiriki " Amefafanua Mbelwa.
Aidha, Mbelwa,amesema kuwa licha ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi lakini pia malengo mengine ni kuhamasisha jamii juu ya masuala mazima ya usafi wa Mazingira na upandaji wa miti.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa