MKUU wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. MussaKilakala, amesema Manispaa ya Morogoro inatarajia kuchonga zaidi ya Km 90 za barabara ili kuondoa changamoto ya barabara ambapo imekuwa kilio cha muda mrefu kwa Wananchi.
Hayo ameyasema Julai 16-2025 akizindua rasmi zoezi la uchongaji wa barabara Kata ya Lukobe Mtaa wa Tuelewane.
Akizungumza na Wananchi waliojitokeza katika Uzinduzi huo wa uchongaji wa barabara, DC Kilakala, ameishukuru Manispaa ya Morogoro Kwa uamuzi wa kuja na muarubaini wa kero za miundombinu ya barabara kwa kununua Greda kupitia mapato ya ndani.
DC Kilakala, amesema Manispaa yaMorogoro imekuwa na changamoto kubwa ya miundombinu ya barabara hivyo Gredahilo litakuwa ni muarubaini wa kero za miundombinu ya barabara kwa Kata zote 29za Manispaa ya Morogoro.
Aidha, DC Kilakala, amewataka wataalamu kulitumia Greda hilo kwa malengo yaliyokusudiwa ili Wananchi waendelee kunufaika na matunda ya Kodi zao.
" Leo tumezindua Mradi wetu wakuchonga barabara, nitoe wito kwa wananchi na Viongozi wa Mitaa tutoeUshirikiano ili kulinda mtambo huu na kuepuka kukwamisha shughuli za mradiunaoendelea kwani tukikwamisha mradi huu , tutakuwa tumekwamishaMaendeleo ya Wananchi wetu" Amesema DC Kilakala.
Kwa upande wa Kaimu Mkurugenzi waManispaa ya Morogoro, Christopher Komba, amesema greda hili limenunuliwashillingi bilioni 1.3 kupitia mapato ya ndani, hivyo matarajio yake kuonalinakwenda kutatua changamoto ya barabara na kurahisisha mawasiliano ya usafirikwa Wananchi.
Naye Kaimu Meneja wa Tarura Manispaaya Morogoro, Eng. Boniface Kapumbe, amesema zoezi la uchongaji wa barabaralinafanywa na taasisi ya Tarura kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkurugenzi waManispaa ya Morogoro.
Kapumbe , amesema kuwa zoezi hilolitaenda kwa awamu ambapo kila Kata Mtambo huo utapita kwa ajili ya kutatuachangamoto ya barabara.
Upande wa mwananchi Mtaa wa TuelewaneKata ya Lukobe, ameishukuru Manispaa ya Morogoro Kwa kutatua kero ya barabaraambapo barabara ya Mtaa huo ilikuwa changamoto na Sasa wanaamini uchongaji wabarabara hiyo itawarahisishia Wananchi huduma ya usafiri kwa urahisi.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa