MANISPAA ya Morogoro imegawa vitabu 45,486 kwa Waalimu wa shule za Msingi kwa ajili ya kuwafundishia wanafunzi.
Vitabu hivyo vimetolewa Februari 05/2023 katika Ofisi Kuu ya Manispaa ambapo kwa kila shule walikuwepo wawakilishi kwa ajili ya kupokea vitabu hivyo.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi vitabu hivyo, Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Morogoro , Chausiku Masegenya, amewataka waalimu na wanafunzi kutumia vitabu hivyo kwa kuvitunza kwa lengo la kutumika kwa muda mrefu wakati wa masomo yao na kuamini kwamba vitabu hivyo vitaleta ufanisi katika kukuza uelewa wa wanafunzi na kuweza kufanya vizuri katika masomo yao.
Aidha, Chausiku, amewataka walimu wa shule kufuatilia kwa makini wanafunzi wote watakaopatiwa vitabu hivyo ili visipotee.
Miongoni mwa vitabu hivyo ni vitabu vya kiada darasa la kwanza na la pili 23,086, vitabu vya hadithi vyenye ukubwa wa A4 vikiwa 20,175 na vitabu vya hadithi vyenye ukubwa wa A3 vikiwa 2,225.
" Tunaishukuru Serikali chini ya Rais wetu , Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kutupatia vitabu hivi, tunaamini lengo la Serikali kutupatia vitabu hivi ni kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji kwa waalimu ili kukuza viwango vya elimu , tunaomba waalimu mkavitunze vizuri" Amesema Masegenya.
Kwa upande wa Afisa Elimu vifaa na takwimu elimu Msingi, Amna Kova, amewataka waalimu kuvitunza vitabu hivyo ili viendelee kusaidia vizazi vijavyo huku akiwataka waalimu kuona umuhimu huo na kusimamia kwa faida ya kuongeza tija katika ufundishaji.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro
Anuani: 166 morogoro
Simu: 0232614727
Simu: 0734-039300
Baruapepe : info@morogoromc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Halmashauri ya Manisaa ya Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa